ZAIDI YA MILIONI TANO ZATUMIKA KUNUNUA VIFAA MAABARA NSIMBO ,WAZAZI WATAKIWA KUTOWAZUIA WATOTO KUSOMA SAYANSI
Na.Issack Gerald -Nsimbo Katavi
Wazazi na walezi katika Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi wametakiwa kutowazuia watoto wao kupata fursa ya elimu.
Wito huo wa kuwataka wazazi na walezi kutowazuia watoto wao kupata fursa ya elimu hasa katika masomo ya Sayansi umetolewa na Diwani wa kata ya Machimboni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu,afya na Maji Halmashauri hiyo Raphael Kalinga wakati akikabidhi vifaa vya maabara tatu za Sayansi katika Shule ya Sekondari Machimboni iliyopo kata ya Machimboni kwa niaba ya waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda.
Naye Kaimu Mkurugenzi Halmshauri ya Wilaya Nsimbo Michael Nzyungu amesema vifaa hivyo vimegharimu Shilingi milioni tano na laki nne ambapo maabara hizo zitazinduliwa na Mwenge wa Uhuru utakapowasili keshokutwa Julai 17 katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambapo pamoja na mambo mengine wanafunzi wakitakiwa kuvitunza vifaa hivyo.
Wakati huohuo wazazi kata ya
machimboni wamesema kuletwa kwa vifaa vya maabara katika shule hiyo kutaongeza
kiwango cha ufaulu wa wanafunzi shuleni hapo.
Vifaa hivyo vinakabidhiwa katika
uongozi wa Shule ya sekondari Machimboni ukiwa zikiwa ni wiki tatu tangu
maabara hizo kutakiwa ziwe zimekamilika hadi kufikia Juni 30 mwaka huu kama
utekelezaji wa agizo la Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete.
Hata hivyo mbali na Gharama ya vifaa
hivyo kutajwa,gharama iliyotumika katika ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara
haijatajwa.
Comments