Posts

RAIS MAGUFULI AMTEUA MWENYEKITI WA BODI YA TAIFA YA WAHASIBU NA WAKAGUZI WA HESABU (NBAA)

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Isaya Jayambo Jairo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA). Kwa mjibu wa Taarifa iliyotolewa leo na katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Prof. Jairo unaanza leo tarehe 11 Aprili,2018. Prof.Jairo ni Mkuu wa Chuo cha Kodi (ITA) na ameteuliwa kushika wadhifa huo kwa kipindi cha pili baada ya kipindi chake cha kwanza kumalizika. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com

AJALI YA TRENI KATAVI

Image
Mabehewa 4 ya Treni ya mizigo ambayo ilikuwa ikisafiri kutoka Wilayani Mpanda Mkoani Mpanda Katavi kuelekea Tabora yameacha njia na kuanguka. Afisa Uhusiano Shirika la Reli  Mohamed Mapondela  amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo amesema mabehewa hayo yameangukia katika eneo la Shankala mkoani Katavi. Amesema hakuna mtu aliyejeruhiwa wala uharibifu wa mali na kinachoendelea kwa sasa kutoa mizigo na kuweka sawa njia ya treni ili kuruhusu safari ziendelee kama kawaida. Kwa upande mwingine Bw.Mapondela hakueleza sababu hasa zilizosababisha ajali hiyo kutokea lakini amesema huenda   ikawa imechangiwa na uchakavu wa njia hiyo ya treni. Reli hiyo inayotajwa kuwa ni miongoni mwa reli kongwe zilizojengwa nchini enzi za ukoloni miongo kadhaa iliyopita.   Habari zaidi ni  www.p5tanzania.blogspot.com

MKOANI KATAVI AHUKUMIWA JELA KWA KUMILIKI RISASI ZA SILAHA YA KIVITA

Image
Mahakama ya wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imetoa hukumu dhidi ya Bw.Kigalu Huba(25) mkazi wa kijiji cha Kambuzi wilayani Mpanda Mkoani Katavi aliyekuwa akituhumiwa kwa kosa la kukutwa na risasi 12 za silaha AK-47 ya kivita ambapo mahakama hiyo imemuhukumu kwenda jela miaka 20. Hakimu mkazi wa mahakama   hiyo Mh.Chiganga Tengwa akitoa hukumu hiyo leo amesema mahakama imejiridhisha bila kuacha shaka kuwa alitenda kosa hilo baada ya kusikiliza shadi wa pande zote ambazo ni mtuhumiwa na upande wa Jamhuri ambao ni serikali. Awali upande wa Jamhuri ambayo ni serikali wamesema Bw. Kigalu Huba   alikutwa na risasi hizo Machi 19,2018 ambapo ni kinyume na kifungu cha sheria namba 7 ya mwaka 2015 kinachohusu umiliki wa silaha   huku wakiiomba Mahakam itowe adhabu kali kwa mtuhumiwa ili iwe wenye tabia kama hiyo. Kwa upande wake Bw.Huba akitoa utetezi wake mahakamani hapo ameiomba mahakama kumpunguzia adhabu aliyopewa akisema kuwa anategewa ana mke na watoto watatu na asipop...

RC RUKWA AFANIKISHA ENEO LA UJENZI WA NYUMBA ZA POLISI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amefanikisha kupatikana kwa ekari 3 ili kujengwa kwa nyumba za askari polisi katika eneo la karibu na kituo cha polisi kipya kinachomaliziwa kujengwa katika kata ya Mtowisa,Wilayani Sumbawanga na kurahisisha makazi ya polisi katika bonde la ziwa Rukwa. Hayo yamejiri ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya wananchi wa kata ya Mtowisa kwa Mkuu wa Mkoa waliyoiahidi tarehe 13.11.2017 Mh.Wanagabo alipofanya ziara katika eneo hilo na kudai kuwa usalama wa bonde hilo sio mzuri kwa kukosa kituo bora cha polisi na makazi yao na kupelekea kuanzisha ujenzi wa kituo na hatimae kuomba nguvu ya Mkuu wa Mkoa kuweza kumalizia ujenzi huo. Mtendaji wa Kata ya Mtowisa Paulo Katepa alimuhakikishia MKuu wa Mkoa kuwa eneo hilo limeshapatikana na tayari kwa kukabidhi kwa askari polisi kwaajili ya taratibu nyingine za kisheria na kumuhakikishia kuwa eneo hilo halihitaji fidia ya aina yoyote na kwamba wananchi wa Kijiji cha Mtowisa wameridhia bila ya kusukumwa, na ...

WAKAZI WALALAMIKA KITUO CHA AFYA KUKOSA CHUMBA CHA KUHIFAHIDHIA MAITI

Image
WAKAZI wa kata ya mtowisa wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa wamelalamikia kitendo cha kituo cha afya Mtowisa ambacho ni kikongwe kwa zaidi ya miaka 20 kutokuwa na chumba cha kuhifadhia maiti kitendo kinachosababisha wagonjwa kukaa na maiti muda mrefu wodini baada ya mtu kufariki. Wakizungumza mbele ya mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo alipokuwa katika ziara yake ya kikazi na kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji hicho.  Wakazi hao walimweleza mkuu huyo wa mkoa kuwa wagonjwa wanalazimika  kulala na miili ya marehumu wardini  huku wakisubiri ndugu wa marehamu kufika na kuchukua miiili hiyo kwa maziko na wakati mwingine maziko ya baadhi ya watu yamekuwa yakifanyika haraka bila kusubiri ndugu wa karibu na marehemu hao kutokana na kuzikwa mapema kwa kuhofia kuharibika kutokana na  kukosekana chumba cha kuhifadhia maiti. Mmoja wa wakazi hao  Christina Mponji alisema kuwa iwapo kifo kikimfika mgonjwa aliyekuwa amelazwa jirani na kitanda ch...

MAHAKAMA KUTOA HUKUMU KESHO MKOANI KATAVI

Image
Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Mh.Chigangwa Tengwa amesema kesho Aprili 10,2018 inatarajia kutolewa hukumu dhidi ya Kigalu Huba mkazi wa kijiji cha Kambuzi Halt wilayani Mpanda Mkoani Katavi anayekabiliwa na kosa la kukutwa na risasi 12 za silaha aina ya kivita   ya AK47. Mh.Tengwa amefikia uamuzi huo leo baada ya kusikiliza mashahidi wa pande zote mshtaki na mshtakiwa. Awali mkuu wa mpelelezi mkoani Katavi Emmanuel Parangyo ameiambia mahakama hiyo kuwa Bw.Humba alipatikana na hatia hiyo Tarehe 19 Machi,2018   katika nyumba anayoishi. Aidha Parangyo ameiambia mahakama kuwa mwananchi haruhusiwi kumiliki risasi au silaha ya kivita kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria za nchi ya Tanzania. Mmoja wa mashuhuda upande wa washtaki akiwemo Mwenyekiti wa kijiji cha Kambuzi Halt Bw.Tuamin Elly,Bw.Huba alikuwa akilalamikikiwa na wananchi kwa kujihusisha na matukio ya uhalifu mara kwa mara. Hata hivyo mtuhumiwa amekana mashtak...

MAOFISA WA JESHI LA POLISI 458 WATIMULIWA KAZI

Image
Jumla ya maofisa wa Jeshi la Polisi wapatao 458 wamefukuzwa kazi kutokana na utovu wa nidhamu kuanzia mwaka 2015 hadi Machi mwaka huu. Kauli hiyo imetolewa jana Aprili 7 na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro alipokuwa akizungumza mbele ya Rais John Magufuli wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za Polisi na ufunguzi wa kituo cha Polisi cha Utalii na Kidiplomasia jijini Arusha. Sirro alisema kazi ya Jeshi la Polisi ni kurekebisha mienendo ya wananchi, hivyo kabla hawajawaelimisha wananchi wanapaswa kuwa na mienendo mizuri wao kwanza. Alifafanua kwa kulitambua hilo ndiyo maana askari waliokwenda kinyume na azma hiyo walichukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kazi, ambapo kwa mwaka 2015, 198 walifukuzwa kazi. Alisema kwa mwaka 2016 walifukuzwa askari 165, 2017 (81) na kuanzia Januari hadi Machi mwaka huu wamefukuzwa askari 14. Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com