MAGUFULI ATEUA MWANASHERIA MKUU MPYA WA SERIKALI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amemteua Dokta Adelardus Kilangi kuwa Mwanasheria mkuu wa serikali. Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Rais wa Tanzania John Magufuli Kabla ya uteuzi huo Dokta Kilangi,alikuwa Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino,kituo cha Arusha na pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Shughili za mkondo wa juu ya mafuta-PURA. Wakati huohuo,Rais Magufuli amemteua Paul Ngwembe kuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Paul Ngwembe,Mkurugenzi wa masuala ya sheria katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania. Kufuatia uteuzi huo,Rais Magufuli amewateua aliyekuwa Mwanasheria mkuu wa serikali George Mcheche Masaju na Aliyekuwa Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali Gerson Mdemu kuwa Majaji wa Mahakama kuu. Uteuzi huo pia umeanza jana Februari mosi. Jana Rais Dkt.John Magufuli alisema bado kuna tatizo kubwa katika ofisi ya DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka) na AG (Mwanasheria Mk...