Posts

DC MPANDA ATAKA VIONGOZI NGAZI ZOTE KUSHIKAMANA PAMOJA KUSUKUMA GURUDUMU LA MAENDELEO-Julai 31,2017

MKUU wa Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Bi.Lilian Matinga,amewataka viongozi wote wilayani Mpanda kushikamana kwa pamoja katika kusukuma maendeleo ya Mkoa wa Katavi.

WAKAZI WILAYANI MPANDA WALALAMIKIA SERIKALI KUHUSU SHIRIKA LA MAENDELEO YA PETROLI TANZANIA (TPDC) KUTUNZA KICHAKA MTAA WA MSASANI KWA MIAKA 25 BILA KUENDELEZA MRADI NA HATIMAYE KICHAKA HICHO KIMEGEUKA KUWA MAFICHO YA VIBAKA NA WEZI-Julai 31,2017

WAKAZI wa Mtaa wa Masasani Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wamelalamikia hatua ya eneo la uwekezaji wa shirika la maendeleo ya Petrol Tanzania TPDC kuwa maficho ya uharifu kutokana na eneo hilo kuwa kichaka baada ya kutoendelezwa kwa zaidi ya miaka 25 sasa.

MKUU WA WILAYA YA MPANDA ATAKA WANANCHI WASIUZE CHAKULA OVYO KUEPUKA BAA LA NJAA-Julai 30,2017

Mkuu wa wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi Bi. Lilian Charles Matinga ametoa wito kwa wananchi wilayani Mpanda kutunza chakula walichovuna katika msimu huu ili kujiepusha na baa la njaa linaloweza kujitokeza.

HALMASHAURI YA WILAYA YA MPANDA YATENGA ENEO LA UJENZI SHULE SEKONDARI YA KATA YA KASEKESE-Julai 30,2017

Image
Mkuu wa Wilaya Tanganyika Salehe Mhando akisaini katika daftari la wageni  Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi,imetenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya kata katika kata ya kasekese wilayani humo. 

RUSHWA YA SHILINGI ELFU 15,YASABABISHA MUUGUZI WA HOSPITALI KUSIMAMISHWA KAZI-Julai 28,2017

Image
Mkuu wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya, Rehema Madusa, amemsimamisha kazi mtumishi wa Hospitali ya Wilaya kwa tuhuma za kudai na kupokea rushwa ya Sh. 15,000 kutoka kwa mzazi ili amtibu mtoto wake.

PROFESA LIPUMBA ASHTAKIWA NA WABUNGE ALIOWATIMUA-Julai 28,2017

Image
Prof.Ibrahim Lipumba Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof. Lipumba  Siku chache baada ya kuwavua uanachama Wabunge wanane wa Viti Maalum kisha Spika Ndugai kuridhia uamuzi huo,jana July 27, 2017 Wabunge hao wamefungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

WATANZANIA 96 WAFADHILIWA KIMASOMO NA NCHI YA UHOLANZI-Julai 28,2017

Kwa mwaka 2017/18 Watanzania 96 wamepata nafasi za kusoma katika Vyuo vyenye ubora wa juu nchini Uholanzi ambapo nafasi 54 kati ya hizo ni kwa ngazi ya Shahada ya uzamili na 42 watasoma kozi fupi inchini humo.