WAKAZI KITONGOJI CHA KAMINI HALMASHAURI YA NSIMBO WAOMBA OPARESHENI YA KUWAONDOA KATIKA ENEO LA HIFADHI ISITISHWE.
Na.Issack Gerald-Mpanda-Januari 30,2017 WAKAZI wa kitongoji cha Kamini kilichopo kata ya Ugalla wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wamwasilisha barua katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo wakiomba Oparesheni ya kuwaondoa katika kitongoji hicho isitishwe kwa madai kuwa mipaka kati ya kitongoji hicho na misitu ya hifadhi haikufuata taratibu na mipaka kukosewa.