HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO YAOMBA KUIDHINISHIWA SHILINGI BIL.24.9 MWAKA WA FEDHA 2017/2018
Na.Issack Gerald-Nsimbo Katavi
HALMASHAURI ya Wilaya ya Nsimbo Wilayani
Mpanda Mkoani Katavi,imeomba kuithinishiwa na serikali kuu shilingi Bilioni
24,886 ,569,000.
Kiasi hicho cha fedha kimepitishwa na
baraza la madiwani katika kikao chake maalumu cha kupanga makadirio kwa mwaka
wa fedha 2017/2018 ili kiasi hicho kitumike kwa ajili ya miradi ya maendeleo
katika halmshauri hiyo iliyokusudiwa kikao ambacho kimefanyika katika ukumbi wa
Halmashauri hiyo.
Afisa uchumi wa Halmshauri ya Wilaya
ya Nsimbo Bw.Jabir Chilumba,akisoma bajeti katika kikao hicho amesema kuwa
bajeti hiyo itakapopitishwa serikalini Shilingi Bilioni 9.6 sawa na asilimia 39
zitatumika kulipa mishahara ya watumishi,Shilingi bilioni 2.1 sawa na asailimia
8% kwa matumizi ya kawaida huku shilingia bilioni 12.3 sawa na asilimia 50
zikitumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Katika kikao hicho maalumu cha baraza
hilo ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo,aidha
Bw.Chilumba amesema mapato ya ndani yanatarajia kuwa bilioni 1, 500,047,000.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mh.Raphael Kalinga pamoja na kulipongeza baraza
kwa kupitisha bajeti hiyo ya mwaka wa fedha 2017/2018 amesema miradi ya maji
imetengewa shilingi bilioni 4,387,999,676 ambapo kati ya kiasi hicho shilingi 4,187,999,676
zinatoka benki ya dunia na Shilingi Milioni 200 kutoka Tamisemi.
Aidha Mh.Kalinga mbali kutoa wito kwa
viongozi Ngazi ya Vijiji hadi kata kutumia fedha wanazozipokea kwa malengo
yaliyokusudiwa pia amesema halmashauri inategemea kipato kwa kiasi kikubwa
kutoka vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na migodi,minada na miara ya simu.
Wakati huo huo wakati madiwani
wakisema kuwa bajeti imekidhi mahitaji ya miradi ya maendeleo katika halmshauri,kwa
upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.Mwailwa
Smith Pangani amesema makadirio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018
yamezingatia mahitaji ya wananchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo kwa
mwaka wa fedha 2016/2017 ilikuwa imekisia kukusanya Shilingi Bilioni 1.3 ambapo
hata hivyo kwa mwaka huo ilikusanya shilingi 625 ambapo kwa mwaka 2017/2018 halmashauri
imekadilia kukusanya bilioni 1.5 sawa na ongezeko la asilimia 12.38 kwa mwaka
2016/2017.
Halmashauri imepanga kushughulikia
vipaumbele vya maji,afya barabara na elimu katika bajeti zake.
Pata habari hii pia kupitia
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments