TANZANIA NA UHORANZI ZASAINIANA MKATABA WA KUWEKA UMEME WA UHAKIKA MKOANI KATAVI,ZAIDI YA VIJIJI 15 KUNUFAIKA
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi
SERIKALI za Tanzania na Uhoranzi kwa
pamoja zimesainiana Mkataba wa Shilingi Bilioni 44/= ili kufanikisha ukamilika
kwa mradi wa umeme wa uhakika Mkoani Katavi ifikapo mwezi Juni mwaka 2017.
Mashine zinazofua umeme |
Hayo yamebainishwa na Meneja Taneco
Mkoni Katavi Mhandisi Julius Sabu wakati akitoa taarifa ya hali ya umeme katika
Mkoa wa Katavi kupitia kikao cha baraz ala madiwani.
Amesema kuwa katika kutatua matatizo
ya kukosekana kwa umeme,Tanzania kwa kushirikiana na serikali ya Uhoranzi
wamesainiana mkataba wa Shilingi Bilioni 44 ili kuweka umeme wa uhakika Mkoani Katavi ambapo kila
upande umechangia shilingi bilioni 22 kupitia mradi wa ORIAL.
Mhandisi Sabu pia amesema katika
hatua ya awali jumla ya mashine 2 zinazozalisha umeme wa Kilowati 1200 sawa na
Megawati 2.5 zinatarajiwa kufungwa ili kuzalisha umeme ni katika mradi huo wa
ORIAL ambapo mpaka mradi utakapokamilika Mei 30 mwaka 2017 mashine 4
zinazotakiwa zitakuwa zimefungwa mashine 4.
Aidha amesema Mkandarasi wa Mradi wa
ORIAL amekwishaanza kushughulika na mradi.
Katika mardi wa umeme wa ORIAL unatarajia
kunufaisha vijiji 15 vya Mkoa wa Katavi ambavyo ni Magamba ,mtisi,Matandala ,Sitalike,kakese
mbugani, Kalilankulukulu, Ifukutwa, majalila, Igalula,Kabungu,na shule ya
Sekondari Mpanda.
Hata hivyo Kwa upande wake Shirika la
umeme nchini Tanesco kwa sasa imetenga bajeti ya shilingi mil 350,888,669/= ili
kupeleka umeme wa uhakika mara baad aya vifaa kuwasili Mkoani Katavi ambapo
umeme huo utapelekwa katika maeneo ya Kasimba, misengeleni, Kazima, kilimahewa,
Misunkumilo, Kichangani,Mpanda girls na Makanyagio.
Wakati huo huo Shirika la Tanesco baada
ya kuwasilishwa kwa vifaa vya umeme hivi karibuni katika miradi mipya ambayo
imepangwa,maeneo ya Kapalangao, Shanwe, Misengeleni, Misunkumilo,Nsemulwa,Kazima
na Mpanda Hotel maeneo ya viwandani ambayo imetengewa shilingi milioni 525,769,846/=.
Mradi wa ORIAL hapa nchini unakuja
kutekelezwa Mkoani Katvi baada ya kukamilika katika Wilaya za Ngara na
Biharamulo zilizopo Mkoani Kagera
Hata hivyo shirika la kuzalisha umeme hapa nchini TANESCO mkoani Katavi limesema tatizo
la kukatika kwa umeme mara kwa mara kutokana na uchakavu wa Mashine
zinazozalisha umeme zilizopo.
Kwa sasa mashine zinazotumika zilihamishwa kutoka Shinyanga na Njombe mwaka 1992
na 1994 ambapo mpaka sasa amshine zilizopo zimetumika kwa zaidi ya miaka 40.
Endelea kuhabarika zaidi na P5 TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments