2017 MWENGE KUWASHWA MKOANI KATAVI KUZIMIWA ZANZIBAR
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama
UZINDUZI wa mbio za Mwenge kwa mwaka
2017 unatarajia kufanyika Mkoani KATAVI na kilele cha mbio za mwenge huo
kitafanyika Zanzibar.
Kwa mwaka 2016 mbio za mwenge wa uhuru
zilizinduliwa Mkoani Morogoro na Mgeni rasmi akiwa makamu wa Rais wa Tanzania
Mh.Samia Suluhu Hassaan kilele cha mbio Za mwenge wa uhuru kimefanyika Mkoani
Simiyu na mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa.baraza la
mapinduzi ya Zanzibar Dkt Ally Mohamed Shein.
Mwenge wa
Uhuru kwa mwaka 2016 umekimbizwa katika siku 179 ndani ya Mikoa 31 na
Halmshauri 179 za Tanzania
Kauli mbiyu kwa mwaka 2016 ilikuwa inasema hivi ’’Vijana ni nguvu kazi ya taifa,washirikishwe na kuwezeshwa’’.
Kauli mbiyu kwa mwaka 2016 ilikuwa inasema hivi ’’Vijana ni nguvu kazi ya taifa,washirikishwe na kuwezeshwa’’.
Endelea kuhabarika na P5 TANZANIA
Mawasiliano : p5tanzania@gmail.com
Comments