MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI KUFANYIKA LEO 1/10/2016
Na.Issack Gerald
Bathromeo Mashama
Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, imesema leo inaadhimisha kilele cha
Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani.
Kwa mjibu wa
Msemaji wa Wizara hiyo Bw. Erasto Ching’oro amesema Katika siku hii,Tanzania
inaungana na nchi nyingine wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha Siku hii
kwa mujibu wa Azimio la Umoja wa Mataifa Na. 49 la mwaka 1991.
Maadhimisho
ya siku ya wazee duniani ni moja kati ya jitihada za Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa (UN) katika kutambua na kuhamasisha jamii kuweza kulinda na
kutetea haki za wazee duniani kote.
Umoja wa
Mataifa umetenga siku hii kwa lengo la kutafakari hali ya maisha ya wazee na
changamoto zinazowakabili wazee; na hivyo kuweka mipango thabiti ya kuboresha
maisha yao na kuwafanya waishi maisha ya heshima, hadhi, na kuthaminiwa utu
wao.
Jamii, na wadau wengine wameaswa kutafakari na kuweka mikakati ya kukabiliana na vitendo vya ukatili,
mauaji, ubaguzi na dhuluma dhidi ya wazee; vitendo ambayo ni kinyume dhidi ya
haki za binadamu.
Maadhimisho
haya kwa mwaka 2016 yanafanyika Kitaifa katika wilaya ya Mbalali, mkoani Mbeya.
Kilele
cha maadhimisho haya kitajumuisha shughuli mbalimbali ikiwemo huduma ya upimaji
wa hiari wa afya na ushauri kwa wazee, michezo na maonesho ya bidhaa na kazi
mbalimbali zinazofanywa na wazee.
Katika
kipindi hiki cha Maadhimisho hatuna budi kuenzi na kudumisha mila na desturi
nzuri za kuwaenzi wazee kwa kutambua kuwa wazee ndiyo chanzo cha urithi wa
historia ya nchi, washauri wa familia na jamii, watu wenye hekima, na walezi
katika jamii.
Hivyo
jamii inaowajibu wa kuwaondolea vikwazo wazee katika kupata huduma za kijamii
ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua pale ambapo
mzee ananyanyaswa au kutendewa
isivyostahili.
Kauli mbiyu ya mwaka huu 2016 INASEMA “Zuia
Unyanyasaji dhidi ya Wazee”.
Pata habari hii pia
kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa Ushauri au maoni
tuma kupitia p5tanzania@gmail.com
Comments