ASILIMIA 45 YA WATOTO CHINI YA MIAKA 18 TANZANIA HUPATA UJAUZITO NA KUPOTEZA MAISHA WAKATI WA KUJIFUNGUA
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama
-Nkasi Rukwa
Asilimia 45 ya watoto wa kike waliochini ya
umri wa miaka 18 hupata ujauzito na kupoteza maisha kila mwaka wakati wa
kujifungua kwa mjibu wa utafiti uliofanywa na Shirika lisilokuwa la
kiseriklai la Plan International Tanzania.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji
wa Shirika la Plan intenational Tanzania Gelard Magashi wakati wa
zoezi la uzinduzi wa mpango wa kuzuia ndoa za utotoni lililofanyika
wilayani Nkasi Mkoani Rukwa katika ukumbi wa St.Bakhita Chuo cha uuguzi
Namanyere
Magashi alieleza kuwa,zaidi ya watoto 16,000
elfu wapo katika ndoa za utotoni katika mikoa ya Morogoro,Rukwa na
Shinyanga,hali ambayo imekuwa ni tatizo kubwa ambalo limekuwepo katika
jamii nyingi hapa nchini huku likionekana kutotiliwa maanani ikiwemo
kutochukuliwa hatua madhubuti kwa wahusika.
Aidha alizungumzia changamoto kubwa iliyombele yao
katika mapambano ya kuzuia mimba za utotoni kuwa ni pamoja na mila
na desturi kwa baadhi ya makabilia hapa nchini,umasikini,uelewa na mtazamo
finyu kwa jamii kuwa mtoto wa kike ni kitegauchumi kwenye familia ,
Aidha alifafanua kuwa,mradi huo unatekelezwa katika
wilaya ya kilombero mkoa wa morogoro na Nkasi wilayani Rukwa kuanzia mwaka huu
wa 2016,hadi mwaka 2019 ambapo unalenga kufanya kampeni mbalimbali
zitakazowezaesha kuondoa tabia za kuozesha watoto wadogo wenye chini ya umri wa
miaka 18.
Kwa upande wake meneja wa mradi huo wilaya ya
Nkasi William Mtukananje alisema ,plan
international imejikita kuangalia maeneo mhimu ikiwemo Afya ya mama na
mtoto,maji na usafi wa mazingira pamoja na ulinzi na usalama wa mtoto
ambapo wanatarajia kuanzisha mradi wa Afya katika wilaya ya nkasi ifikapo Januari
2017 ili kutoa huduma za kiafya kwa mama na mtoto kwa ukaribu na ufanisi zaidi.
Kwa upande wake Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi
huo Naye Vicent Magendela ambaye ni Afisa mtendaji mamlaka ya mji mdogo
Namanyere kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Nkasi Said Mohammed
Mtauda,alisema shirika plan international Tanzani kwa ujio wao
wilayani ni muhimu kutokana na kuwa takwimu zinaonyesha
aslimia 40% katika wilaya ya nkasi watoto wanaathiriwa na ndoa za utotoni.
Magendela alisema,serikali inafanya kila jitihada
kuhakikisha miundombinu ya mama katika kujifungua ikiwemo dawa hospitalini
pamoja na mazingira ya kujifungulia yanaboreshwa ili kuepuka vifo vya mama na
mtoto wakati wa kujifungua.
Mratibu wa plan international wilayani Nkasi Nestory
Frank alitoa wito kwa wazazi na walezi kuwa, kila mmoja anawajibu katika
kufanikisha malengo ya mradi huo, huku akiyataja baadhi ya madhara ya
ndoa za utotoni kuwa ni pamoja na watoto kunyanyasika kijinsia ,kiakili,kimwili
pamoja na kuwa hatarini kupoteza maisha wakati wa kujifungua sababu ya kutokwa
damu nyingi wakati wa kujifungua kwa kuwa viungo vyao vinakuwa bado havijawa
tayari kuhimili kuzaa.
Kauli mbiyu ya Plan Itnernational Tanzania inasema ni
“plan, watoto kwanza”.
Pata habari hii pia
kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa Ushauri au maoni tuma kupitia p5tanzania@gmail.com
Comments