WAKAZI WILAYANI TANGANYIKA WAAGIZWA KUONGEZA KASI YA KUJENGA SEKONDARI KILA KATA
Na.Issack Gerald Bathromeo
Mashama-Tanganyika
WAKAZI wilayani Tanganyika Mkoani
Katavi kwa Kushirikiana na uongozi wa vijiji na kata katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika,wameagizwa
kuweka mikakati ya ujenzi wa shule za Sekondari kila kata ,ili kila mwanafunzi
asome bila kuhangaika na badala yake apate elimu bora.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Saleh Mbwana Mhando akishiriki ujenzi Shule ya sekondari ya Bulamata kata ya Bulamata(PICHA NA Issack Gerald)Septemba 16,2016 |
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika akizungumza na wananchi eneo la kijiji cha Busongola kunakojengwa Shule ya Sekondari Bulamata(PICHA NA.Issack Gerald) Septemba 16,2016 |
Wananchi wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Isubangala kijiji cha Isubangala kata ya Ilangu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya(hayupo pichani)(PICHA NA.iSSACK gERALD) Septemba 16,2016 |
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa
Wilaya ya Tanganyika Bw.Saleh Mbwana Mhando,wakati akizungumza na wananchi
katika mikutano ya Hadhara ambayo ameifanya katika kata za Ilangu na Bulamata.
Aidha Mkuu wa Wilaya ametoa onyo kali
kwa wazazi watakaohusika na kumuoza mtoto wa shule akisema kuwa sambamba na
mwanaume atakayeoa au kumpa ujauzito mwanafunzi
watafungwa miaka 30 bila huruma.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Bulamata
Bw.Godfrey Mbalazi,akisoma taarifa ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Bulamata
inayojengwa katika kijiji cah Busongola ,amesema kuwa ujenzi unaofanyika ni wa
vyumba vitatu na ofisi moj aya walimu ambapo mpaka sasa wamekusanya zaodi ya
shilingi milioni 12 kwa kuanza na ujenzi wa shule hiyo.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka
Ofisi ya Mkuu wa Makazi Mishamo Bw.Harold Boserwe amesema kuwa,wao mpaka sasa
wanasaidia magari kwa ajili ya kusomba maji ,matofali na mawe ili kuharakisha
ujenzi ukamilike ambapo Mkuu wa Wilaya Bw.Mhando amesema kuwa inatakiwa
wanafunzi waanze kusomea katika shule hiyo mwakani.
Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika
ina kata 16 ambapo kati ya hizo kata 6 hazina Shule za Sekondari.
Wakati huo huo,Mkuu wa Wilaya akiwa
katika Shule ya Msingi Isubangala iliyopokata ya Ilangu amezindua vyumba 3 vya
madarasa na ofisi moja ambavyo vimefikia usawa wa renta katika ujenzi ambapo
shule hiyo iliyoanzishwa 17.1.1980 mpaka sasa ina wanafunzi 1071.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya
ameruhusu kufanyika mikutano ya viongozi wa vijiji na kata ilivyokuwa
imezuiliwa na uongozi wa makazi ya mishamo kutokana na mgogoro wa kiutawala.
Katakika taarifa yake Afisa Mtendaji
wa kata ya Ilangu Bw.Seuri Mishileki amesema,mikitano ilikuwa imezuiliwa kwa
takribani wiki mbili mpaka sasa ambapo ameeleza
shughuli nyingi za maendeleo kukwama kutokana na kutokuwepo kwa mikutano
inayowakutanisha viongozi na wananchi.
Chanzo cha Mvutano ni baada ya
mwenyekiti wa kijiji cha Ilangu kujiudhuru na kuvutana kuwa anayechukua nafasi
atoke makazi ya mishamo au upande mwingine.
Habari hii pia ipate
kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments