MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AAGIZA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 200 ZA WAKULIMA WA ZAO LA TUMBAKU CHAMA CHA USHIRIKA TAMCOS KULIPWA NDANI YA SIKU 15.
Na.Issack Gerald Bathromeo
Mashama-Tanganyika
MKUU wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani
Katavi Bw.Saleh Mbwana Mhando,ameuagiza uongozi wa bodi ya Chama cha Msingi cha
Ushirika TAMCOS na Afisa Ushirika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Luxford
Mbunda,kuhakikisha wanalipa zaidi ya
Shilingi milioni 200 wanazodai wakulima wa zao la tumbaku wa Halmashauri ya
Wilaya ya Tanganyika kwa misimu 3 ya kilimo kuanzia mwaka 2011-2015 kabla ya Septemba
30 mwaka huu.
Baadhi ya Wakulima wa Zao la Tumbaku wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika(hayupo pichani) katika Ofisi za TAMCOS Mishamo(PICHA NA.Issack Gerald) |
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Saleh Mbwana Mhando Aliyesimama akihutubia wakulima wa tumbaku wa chama cha Msingi cha Ushirika TAMCOS Mishamo(PICHA NA.Issack Gerald) |
Bw.Mhando ametoa agizo hilo leo katika
mkutano wa hadhara ambao ameufanya baina yake na wakulima wa zao la tumbaku wa Chama cha Msingi cha
Ushirika TAMCOS kilichopo kata ya Mishamo Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika.
Aidha,aMkuu wa Wilaya mesema,serikali
ya Wilaya ya Tanganyika haitamvumilia mtendaji au mtumishi yeyote wa Halmshauri
hiyo,ambaye atasababisha wananchi kunyanyasika katika haki zao,wakati nguvu
kubwa imetumika katika uzalishaji.
Kwa upande wa Meneja wa
TAMCOS,Bw.Valaniho Gataro,Mwenyekiti wa Chama cha Msingi cha Ushirika TAMCOS
Bw.Pridas Amakredo na Afisa Ushirika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ambaye pia
ndiye anayeshughulikia vyama vya ushirika vilivyopo Halmashauri ya Wilaya ya
Tanganyika Bw.Luxford Mbunda,wakijibu hoja za wakulima wa zao hilo katika
Mkutano huo,hoja zao zilikataliwa na wakulima wa hilo kwa madai kuwa majibu ya
madai yao yanajibiwa isivyo.
Wakulima mbali na kudai kiasi cha
zaidi ya Shilingi Milioni 200, zilizotokana na mauzo ya zao la tumbaku,pia
wamedai bodi ya chama cha TAMCOS ivunjwe ili kuchagua viongozi wengine,kwa kuwa
uongozi uliopo madarakani upo kwa ajili ya kuwaibia fedha wanazotakiwa kupewa
wakulima.
Aidha wakulima hao,wamewatuhumu
viongozi wa TAMCOS kuwafutia usajili baadhi ya wakulima wanaoonekana kuhoji
maslahi yao,ambapo baada ya kufutwa imegundulika kuwa wakulima wanazuiwa
kushiriki kilimo cha zao hilo ikiwemo kunyimwa pembejeo licha ya kuwa na haki
ya kupatiwa pembejeo hizo.
Wakati huo huo wakulima wamelalamikia
upandaji miti hewa uliofanywa na mkandarasi aliyepewa tenda ya kupanda miti,
kutokana na malipo ya fedha za wakulima wa Chama Cha TAMCOS licha ya kuwa fedha
alikwishalipwa.
Habari hii pia ipate
kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments