TANESCO NA UFAFANUZI WA TATIZO LA UMEME MPANDA KATAVI
Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
Uchakavu na
ubovu wa mitambo ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa katavi ndiyo imeelezwa
kuwa ndio chanzo kinachosababisha kutokuwa na umeme wa uhakika.
Meneja
mahusiano wa
shirika hilo mkoani Katavi Amon Michael amesema tatizo hilo
litaendelea kuwepo hadi umeme wa msongo mkubwa na mitambo mipya itakapowasili
na kufungwa.
Bw.Michael
amesema uzalishaji wa umeme kwa mkoa ni kilowatt 3200, huku matumizi ya mkoa
ikiwa ni kilowatti 2700 hivyo inapotokea mashine moja ikashindwa kufanya kazi,
umeme unakuwa wa kusuasua.
Aidha Bw.Michael
amewataka wananchi kutumia mafundi wa umeme wanaoshauriwa na shirika hilo ili
kuepuka athari zinazoweza kujitokeza kwa kutumia mafundi ambao hawajasajiliwa.
Hivi
karibubi nyumba Moja iliungua kwa moto kutokana na hitilafu ya umeme ambapo
hata chanzo chake hakijafahamika.
Mhariri :Issack Gerald
Bathromeo
Pata habari hii pia
kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au Ushauri
tuma kupitia p5tanzania@gmail.com
Comments