MWALIMU WILAYANI MLELE AHUKUMIWA JELA MIAKA 30 KWA KUSABABISHA UJAUZITO KWA MWANAFUNZI WAKE
Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mlele mkoani Katavi imemhukumu Mwalimu wa
Shule ya Msingi Ukingwamizi, Une Thom kutumikia kifungo cha miaka 32 jela.
Thom (32) amehukumiwa kifungo hicho baada ya mahakama hiyo kumtia
hatiani kwa makosa mawili ya kumnajisi na kumpatia ujauzito mwanafunzi wake
mwenye umri wa miaka 16.
Msichana huyo ambaye amejifungua mtoto njiti amefariki baada ya kuzaliwa.
Kwa mujibu wa Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Teotimus Swai amesema kwa kuwa adhabu hizo zinaenda
sambamba, mshitakiwa atatumikia kifungo cha miaka 30 jela.
Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Swai amesema mahakamani hapo kuwa
ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka ukiongozwa na Mkaguzi wa Polisi,
Baraka Hongoli umethibitisha kuwa kweli mshtakiwa alitenda kosa hilo.
Mwendesha mashitaka, Mkaguzi wa Polisi, Baraka Hongoli amedai
mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanafunzi
wake huyo kwa muda mrefu hadi akamsababishia ujauzito.
Mhariri :Issack Gerald
Bathromeo
Pata habari hii pia
kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au Ushauri
tuma kupitia p5tanzania@gmail.com
Comments