MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA ATOA AGIZO KWA WATUMISHI WA WILAYA HIYO,ATAKA WAFANYE KAZI KWA WELEDI KWA MANUFAA YA WANANCHI NA KUIEPUKA RUSHWA.
Na.Issack Gerald Bathromeo-Tanganyika Katavi
MKUU wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Saleh
Mbwana Mhando,amewaagiza watumishi wa umma Wilayani Tanganyika,kufanya kazi kwa
weledi na kasi ili kufikia maendeleo yanayohitajika kwa wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika(Mwenye tai) akiwa na baadhi ya watumishi wa Wilaya hiyo baada ya kikao(PICHA NA.Issack Gerald)Septemba 14,2016 |
Baadhi ya watumishi wa idara mbalimbali halmashauri ya wilaya ya Tanganyika katika kikao cha utumishi na mkuu wa Wilaya(Hayupo pichani)(PICHA NA.Issack Gerald)Septemba 14,2016 |
Bw.Muhando ametoa agizo hilo
leo,wakati akizungumza na watumishi wa idara mbalimbali wa Wilaya hiyo,ambapo amewataka
kujiepusha na vitendo vya Rushwa vinavyopelekea kukwamisha kukamilika kwa miradi
ya maendeleo kwa wakati.
Wakati huo huo,Bw.Mhando pamoja na
kutaka utatuzi wa matatizo ya wananchi ulenge katika sekta nyeti ikiwemo huduma
ya maji,afya na elimu pia amewaagiza wakuu wa idara za kilimo kuelekeza nguvu
nyingine katika uanzishwaji wa miradi mingine ya maendeleo itakayoongeza kipato
cha Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika huku katika hatua akiitataka idara ya
misitu ifanye kazi yake ya kukamata wanaoharibu mazingira kwa kukata na kuchoma misitu na ovyo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama
cha Mapinduzi CCM wilayani Mpanda Bw.Beda Katani ambaye pia ndiye kaimu
mwenyekiti wa chama hicho Wilayani Tanganyika,pamoja na kuiomba serikali
kuboresha maslahi ya watumishi kuendana na hali ya maisha kwa sasa yanavyopanda
gjharama,amesema chama kitashirikiana na serikali ipasavyo kuleta maendeleo ya
wananchi ikiwemo kuwafichua wanaokwamisha maendeleo.
Hata hivyo,kwa mjibu wa Mkuu wa
Wilaya ya Tanganyika Bw.Saleh Mbwana Mhando, pamoja na kusema kuwa kikao cha
leo kilikuwa cha kupeana mwelekeo wa namna ya kuleta maendeleo wilayani
Tanganyika kwa kila mkuu wa Idara kwa kuzingatia mahitaji ya mwananchi,pia amesema,hivi
karibuni anatarajia kufanya kikao baina yake na madiwani wa Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika
ili kuelezana namna ya kukamilisha ahadi za serikali ya awamu ya tano katika
wilaya hiyo,ikiwemo pia hata ahadi alizoahidi Rais Magufuli wakati wa kampeni
za uchaguzi wa mwakajana katika mikutano mbalimbali wilayani humo ambazo
hazijaandikwa katika ilani ya chama cha mapinduzi.
Habari hii pia ipate
kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments