KIFO CHA MTU KUJINYONGA KATAVI,NDUGU,MASHUHUDA WASIKITIKA
Na.Issack Gerald
Bathromeo-Katavi
MTU mmoja anaekadiliwa kuwa na umri wa miaka 30 Innocent
Milambo mkazi wa mtaa wa kigoma kata ya Makanyagio wilayani Mpanda mkoani Katavi,amekutwa amekufa kwa
kujinyonga usiku wa kuamkia leo kwa kile
kinachodaiwa kuwa ni imani za kishirikina.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda(PICHA NA.Issack Gerald) |
Kamanda wa polisi Mkoa wa Katavi ACP Damasi Nyanda
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kwamba madaktari wanafanya uchunguzi
katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda ili kubaini chanzo cha kifo hicho.
Aidha kamanda Nyanda ameitaka jamii kuacha kujiadhibu kwa
kujichukulia sheria,mkononi kwani maamuzi yoyote ya kukatisha uhai ni kosa
kisheria.
Nao baadhi ya ndugu,majirani pamoja mashuhuda wa tukio
hilo,mbali na kueleza kusikitishwa na kifo cha Marehemu Innocent
Milambo,wamedai kuwa huenda kuna watu wamehusika na kifo hicho kwa kuwa
inadaiwa kuwa marehemu alianza purukushani nyumbani kwa kuwatishia kuwapiga
waliokuwepo.
Habari hii pia ipate
kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments