WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUWASILI KATAVI KESHO,WANAKATAVI WAOMBWA KUJITOKEZA KUMPOKEA.
Na.Issack Gerald-Katavi
MKUU wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali
Mstaafu Raphael Muhuga ametoa rai kwa
wananchi Mkoani Katavi kujitokeza kwa wingi kumpokea waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa anayetarajia kuwasili kesho kwa ndege Mkoani
Katavi kwa Ziara ya kikazi ya siku nne.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga(PICHA NA.Issack Gerald) |
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majliwa(PICHA NA.Issack Gerald) |
Rai hiyo ameitoa wakati akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu maandalizi ya kumpokea waziri Mkuu
mkoani hapa.
Waziri Mkuu akiwa Mkoani Katavi,atafanya
mikutano mbalimbali ya Hadhara katika Wilaya za Mkoa wa Katavi ikiwemo kutembelea
kijiji cha Majalila kunakojengwa makao makuu ya Halmshauri ya Wilaya ya
Tanganyika na Draja la mto Kavuu lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Kabla ya Waziri Mkuu kuhitimisha
Ziara Agosti 26 mwaka huu akiwa Mkoani Katavi na kurejea Dar es Salaam,Agosti
23 siku ya Alhamisi anatarajia kufanya ziara ya siku tatu Mkoani Rukwa.
Katika hatua nyingine kutokana na tetesi za baadhi ya wanakijiji wa
vijiji vilivyopo mbali na kijiji cha Majalila kilichopo Kata ya Tongwe
kutangazwa kuwa makao makuu ya Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda kuanza kulalamika
kwamba huenda wakakosa baadhi ya huduma kutokana na umbali waliopo,Mkuu wa Mkoa
kupitia Meja Jeneral Muhuga akitolea ufafanuzi kuhusu kijiji cha Majalila kuwa
makao makuu amesema kuwa ni maamuzi yalitokana na vikao mbalimbali
vilivyofanyika kwa nyakati tofauti vikiwemo vikao vya balaza la madiwani na
vikao vya kamati ya ushauri ya Mkoa.
Aidha pamoja na mambo mengine,mkuu wa
Mkoa amesema maamzi yalifanyika ili kumaliza mvutano juu ya makao makuu yanakotakiwa
kuwa na kuondoa vizingiti vya shuhuli zamaendeleo.
Kijiji cha Majalila kilitangazwa
rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali Raphael Muhuga kuwa makao makuu
ya Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika Agosti 4 mwaka huu.
RATIBA KAMILI YA ZIARA YA WAZIRI
MKUU KATAVI-RUKWA
20-8-2016- WILAYANI MPANDA
-Waziri Mkuu anatarajiwa kuwasili jioni
uwanja wa ndege
21-8-2016 HALMSHAURI YA
WILAYA YA NSIMBO(WILAYANI MLELE)
Waziri Mkuu anatarajiwa kutembelea
Ofisi za CCM Mkoa wa Katavi,Atafanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Ndui
Staion yaliyokuwa makazi ya wakimbizi Katumba pamoja nakuzindua mnara mpya
uliojengwa na watanzania wapya wa hapo Katumba kama pongezi kwa Serikali ya
Tanzania kwa kuwapatia uria.
-Waziri Mkuu atafanya mkutano wa
hadhara katika viwanja vya shule ya Msingi Azimio.
22-8-2016 WILAYANI MLELE
- Waziri Mkuu ataanza ziara katika
Wilaya ya Mlele na kuongea na watumishi,kupata taarifa ya mkoa na kufanya mkutano
wa Hadhara.
- Waziri Mkuu atarejea Ikulu Mpanda
Mjini
- Waziri Mkuu taelekea Kijiji cha Majalila Makao Makuu ya
halmshauri na Wilaya Mpya ya Tanganyika
- Waziri Mkuu ataona mradi wa maji majalila
- Waziri Mkuu atafanya mkutano wa hadhara katika kata ya
Mpanda ndogo kasha
-Atarudi Mpanda Mjini Ikulu.
23-8-2016 WILAYANI MPANDA
-Waziri mkuu atafanya mkutano katika
ukumbi wa idara ya Maji ikiwa ni majumuisho ya ziara mkoani Katavi
-Baada ya hapo ataelekea Majimoto
Wilayani Mlele katika Halmshauri ya Wilaya ya Mpimbwe ambapo atafanya mkutano
wa hadhara.
-HATIMAYE ATAELEKEA MKOANI
RUKWA KUENDELEA NA ZIARA MKOANI KUANZIA AGOSTI 23-26,2016.
WILAYANI MLELE-26-8-2016
-Waziri Mkuu atarejea Mkoani Katavi
kuonana na waziri Mkuu Mstaafu katika kijiji cha Kibaoni.
-Baada ya mazunumzo na Waziri Mkuu
Mstafu,Waziri Mkuu atatembelea shule mpya ya msingi Kakuni.
NA HATIMAYE ATAREJEA MPANDA MJINI
KUPANDA NDEGE KUELEKEA DAR ES SALAAM.
Endelea kuhabrika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments