WATANO KATAVI WAHUKUMIWA MIAKA 5-20 KWA TUHUMA ZA NYARA ZA SERIKALI,MWINGINE AACHIWA HURU,WAKILI WAO ASEMA WATAKATA RUFAA
Na.Vumilia Abel-Mpanda
MAHAKAMA
ya wilaya mkoani Katavi imewahukumu watu 5 miaka 5 hadi 20 na mmoja kuachiwa huru waliokuwa wakikabiliwa
na makosa matatu tofauti likiwemo la
kukutwa na nyara za serikali bila kibali.
Akisoma
hukumu hiyo hakimu Chingangwa Tengwa amewataja washtakiwa hao kuwa ni Justini
Baluti,Boniface Hoza,Elias Hoza,Credo Gervas na Sadock Masamba.
Ameongeza
kuwa kosa la kwanza ni kujihusisha na makosa ya uhujumu uchumi,pili ni kukutwa
na nyara za seikali bila kibali na kosa la tatu linamhusu mshtakiwa Boniface
Hoza aliyekutwa na nyara za serikali vipisi 7 vya meno ya Tembo vyenye thamani
ya zaidi ya sh.milioni mia moja.
Kufuatia
hatua hiyo mahakama imewakuta na hatia
washtakiwa wanne waliokuwa wakikabiliwa na kosa la kukutwa na nyara za serikali
vipande 15 vya meno ya tembo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 249
ambao wote watatumikia kifungo cha miaka mitano jela .
Aidha
Chigangwa amesema kwa kosa la pili mahakama imewakuta na hatia washtakiwa
Jastini Baluti na Boniface Hoza wote watatumikia kifungo cha miaka ishirini
jela.
Awali
kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo wakili wa serikali Bw.Wankyo Simon aliomba
mahakamani hapo kutoa adhabu kali kwa washtakiwa ili iwe fundisho kwao na kwa
watu wenyingine.
Nje
ya mahakama baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo wakili wa serikali Simon amesema
ameridhishwa na maamuzi yaliyotolwa na mahakama kama hapa anavyoeleza
Naye
wakili upande wa utetezi uliosimamiwa na Bw.Elias Kifunda amesema kwa kuwa
washatkiwa hawajaridhishwa na maamuzi yaliyotolewa na mahakama wanatarajia
kukata rufaa.
Mhariri:Issack
Gerald Bathromeo
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments