WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUANZA ZIARA KATAVI JUMAMOSI HII,KUTEMBELEA MAJIMBO YOTE MATANO YA MKOA WA KATAVI,SEHEMU YA RATIBA P5 TANZANIA IMEKUSOGEZEA HII HAPA
Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mh.Kassim Majaliwa anatarajia kuanza ziara ya kikazi Mkoani Katavi.
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa |
Mh.Richard Mbogo(mbunge) Jimbo la Nsimbo katika mahojianiano na waandishi
wetu wa habari,amesema kuwa Waziri mkuu akiwa Mkoani Katavi anatarajia
kutembelea jimbo La Katavi
linaloongozwa na mbunge Issack Kamwele (CCM),Jimbo la Kavuulinaloongozwa na mbunge Dk. Pudenciana Kikwembe (CCM)Mpanda Mjini linaloongozwa na
mbunge Sebastian Kapufi (CCM),Jimbo la Mpanda Vijijini linaloongozwa
na mbunge Moshi Selemani Kakoso (CCM) na Jimbo la Nsimbo linaloongozwa
na mbunge Richard Mbogo (CCM).
Mh.Mbogo
amesema Waziri Mkuu Kassim mara baada ya kuwasili Mkoani Siku ya Jumamosi
Tarehe 20 ataanza ziara rasmi siku ya Jumapili Tarehe 21 ambapo ataanzia Jimbo
la Mpanda Vijijini kwa kufanya mkutano majira ya asubuhi katika kijiji cha
Majlila,Jimbo la Nsimbo atafanya mkutano katika Kijiji cha Nduwi Station majira
ya Mchana na mkutano wa tatu utafanyika mkutano Mpanda Mjini katika viwanja vya
Shule ya Msingi Azimio.
Baada ya mikutano hiyo ataendelea na
ziara katika majimbo ya Kavuu,Mpimbwe na Katavi.
Mapema mwezi Februari,20 mwaka huu
kulifanyika kongamano la Maendeleo ya
Rukwa na Katavi lilifanyika Jijini Dar es salaam katika viwanja vya Makumbusho
ambapo akiwa mgeni rasmi katika kongamano hilo,Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliahidi
kuisaidia mikoa ya Rukwa na Katavi kujikwamua katika Shughuli mbalimbali za
maendeleo.
Mpaka kufikia sasa kwa mwaka
2016,takribani Mawaziri wane wamefanya ziara katika Mkoa wa Katavi kusikiliza
kero za wananchi,kuzungumza na wadau mbalimbali wa maendeo,kukagua miradi ya
maendeleo na mengine kuyawekea mawe ya msingi pamoja na kutoa maagizo kwa
viongozi Mkoani Katavi kufanya utekelezaji wa kiutendaji katika shughuli
mbalimbali.
Miongoni mwa Mawaziri ambao
wametembelea Mkoani Katavi ni pamoja na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi
Mh.Mwigulu Lameck Nchemba.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM,Usikose
kitakochoendelea katika ziara ya Waziri Mkuu
Comments