AFISA MTENDAJI WA KIJIJI APEWA WIKI MBILI KUWAONDOA WAKAZI WALIOVAMIA MISITU NA KUFANYA MAKAZI,MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA PIA AZUNGUMZIA ZIARA YA WAZIRI MKUU KATIKA WILAYA YAKE
Na.Issack
Gerald Bathromeo
MKUU wa wilaya ya Tanganyika Saleh
Muhando ametoa wiki mbili kwa Afisa mtendaji wa kijiji cha Mpembe kata ya
Katuma kuhakikisha anawaondoa wananchi waliovamia misitu na kufanya makazi.
Ametoa agizo hilo leo kufuatia
uharibufu mkubwa wa mazingira uliofanywa
na wananchi kwa kufanya shughuli za ukataji miti,uchomaji mkaa na kilimo.
Bw.Mhando amesema ni wajibu wa kila
mwananchi kutunza mazingira ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kutokana na
uharibifu huo.
Ameongeza kusema kuwa mwananchi
yeyote ambaye atakaidi agizo hilo sheria itachukuwa mkondo wake.
Wakati huo huo amewaasa wakazi wa
Wilaya ya Tanganyika kujitokeza kumpokea Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akapoanza
ziara katika Wilaya hiyo Jumapili Agosti 21 mwaka huu.
Aidha amesema kuwa anajisikia furaha
Waziri Mkuu kuanzia ziara katika Wilaya hiyo mara baada ya kuwasili Mkoani
Katavi ambapo anatarajia kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Majalila
kunakojengwa makao makuu ya Wilaya hiyo change kabisa.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM,Usikose
kitakochoendelea katika ziara ya Waziri Mkuu
Comments