WAFANYABIASAHARA MANISPAA YA MPANDA WAPEWA SIKU 6 KUONDOKA MASOKO YASIYO RASMI KABLA YA NGUVU KUTUMIKA.
Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda
WANANCHI wanaofanya biashara katika
masoko yasiyo rasmi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wametakiwa kuondoka na
bidhaa zao wenyewe kwa hiari kabla ya Septemba 5 mwaka huu kuondolewa kwa
nguvu.
Katika Picha Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Nzyungu(PICHA NA.Issack Gerald) |
Miongoni mwa wafanyabishara
wanaopigwa marufuku soko lisilo rasmi lililopo Ujenzi Machinjioni Mpanda hotel.
|
Kauli hiyo imetolewa leo kwa vyombo
vya habari na Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Fransis
Nzungu,kupitia kwa Afisa habari wa Manispaa hiyo Bw.Donald Pius.
Aidha Nzungu amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuzingatia na kuheshimu sheria za mipango miji,kwa kufanya shughuli zao za kila siku katika maeneo yaliyo sahihi ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.
Aidha Nzungu amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuzingatia na kuheshimu sheria za mipango miji,kwa kufanya shughuli zao za kila siku katika maeneo yaliyo sahihi ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.
Mkurugenzi katika taarifa yake
amesema wananchi waliopo katika kata ya Mpanda Hotel,Kawajense na Nsemulwa
wamekuwa wakivunja sheria za mipango miji kwa kuanzisha masoko katika maeneo
yasiyo rasmi na hivyo kuharibu mpango mzima wa Mji wa Mpanda.
Aidha amesema kuanzia Septemba 5
mwaka huu,hataruhusiwa mtu yeyote kufanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi.
Masoko yasiyo rasmi ambayo
wafanyabiashara wametakiwa kuondoka na kwenda katika masoko rasmi ni wanaofanya
biashara maeneo ya Ujenzi Machinjioni na Kawajense Uenyejini.
Kwa upande wa wafanyabiashara
wanaofanya biashara zao eneo la Nsemulwa Migazini,wametakiwa kuhamia kwa muda
kwenye soko lililopo jirani na Tanki la maji hadi hapo watakapooneshwa soko la
kudumu.
Mara kwa mara wafanyabiasahara
wamekuwa wakiulalamikia Uongozi wa Manispaa ya Mpanda kwa kushindwa kuwatengea
masoko ya kufanyia biasahara zao karibu na makazi yao wakisema kuwa wanashindwa
kutekeleza Kauli mbiyu ya Hapa Kazi Tu ya Rais John Pombe Magufuli ili
kujikwamua na umaskini.
Habarika Zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments