MKUU WA WILAYA TANGANYIKA AONYA WATAKAOANDAMANA OPARESHENI UKUTA SEPTEMBA MOSI,ASEMA OPARESHENI UKUTA IWE NI KUJENGA MADARASA,KUTENGENEZA MADAWATI NA SHUGHULI NYINGINE ZA MAENDELEO.
Na.Issack Gerald Bathromeo-Tanganyika
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Mkoani
Katavi Saleh Mbwana Mhando,ametoa onyo kwa wananchi na wanachama wa vyama vya siasa
watakaofanya maandamano ya Opareshen Ukuta katika Wilaya hiyo yanayotarajia
kuanza Septemba mosi.
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyiika Saleh Mhando |
Mkuu wa Wilaya huyo ametoa onyo hilo
wakati akitoa msimamo katika Wilaya yake ikizingatiwa kuwa ndiye mwenyekiti wa
kamati ulinzi na usalama ya Wilaya
akisema kuwa anatekeleza agizo kutoka mamlaka ya ngazi za juu ambao wamezuia
maandamano hayo.
Amesema,jeshi la Polisi Wilayani humo
limejiandaa kuwadhibiti waandamanaji wote watakaoandamana ambapo amesisitiza kuwa
wananchi watumie siku hiyo kufanya shughuli za maendeleo kama ujenzi wa
madarasa,kutengeneza madawati na shughuli nyingine za maendeleo.
Jana Jeshi la Polisi limewakamata
viongozi mbalimbali wa ngazi za juu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema
wakiwemo mwenyekiti wa chama hicho taifa Bw.Freeman Mbowe,aliyekuwa mgombea wa
Urais kupitia chama hicho mwaka 2015 chini ya Mwamvuli wa UKAWA na waziri mkuu
mstaafu wa Tanzania Mh.Edward Ngoyai Lowassa na John Mnyika wakituhumiwa
kufanya vikoa vya ndani vya chama hicho.
Opareshen Ukuta imepangwa kuzinduliwa
nchi nzima ifikapo Septemba mosi mwaka huu huku maandamano yakitajwa kutokuwa
na Ukomo.
Habarika zaidi na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments