JESHI LA POLISI MKOANI KATAVI WAFANYA MAZOEZI KUPAMBANA NA UHARIFU,WANANCHI MITAANI WAKUMBWA NA TAHARUKI.


Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
JESHI la Polisi Mkoani Katavi limetoa onyo kwa watu watakaosababisha ukosefu wa amani katika Mkoa wa Katavi likisema kuwa halitawafumbia macho watu hao na badala yake Jeshi hilo litachukua hatua kali za kisheria kukomesha vitendo vya uharifu.

Kauli hiyo imetolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Damasi Nyanda  wakati Jeshi hilo likifanya mazoezi  mbalimbali likiwemo la ufyatuaji risasi katika viwanja vya Jeshi la Polisi vilivyopo mjini Mpanda.
Kamanda Nyanda amesema kuwa Jeshi la Polisi ni kawaida yake kufanya mazoezi hayo ili kujiandaa kukabili uharifu wa aina yoyote yauharifu utakaojitokeza ambapo amesisitiza kuwa wataendelea kufanya mazoezi muda wowote.
Mapema leo asubuhi baadhi ya wananchi walikumbwa na taharuki mitaani baada ya kiusikia milio ya bunduki wakidhani kuwa kuna uvamizi umetokea kutokana na kuwa wananchi walikuwa hawana taarifa ya ufyatuaji wa risasi kwa leo.
Hatua  ya polisi kufanya mazoezi ya kujiandaa na kupambana na uharifu na waharifu yamepamba moto ikiwa ni siku chache bada ya mauaji ya polisi wanne waliokuwa walinzi wa benki Jijiji Dar es Salaam.
Mhariri : Issack Gerald Bathromeo
Habarika zaidi kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA