TRA RUKWA NA KATAVI YAENDESHA SEMINA KUHUSU MFUMO MPYA ULIPAJI KODI
Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda
WAFANYABIASAHARA mikoa ya Rukwa na Katavi
wametakiwa kutofumbia macho vikwazo vinavyotokana na mfumo mpya wa ulipaji kodi
na badala yake watoe taarifa na maoni ili kuangalia kama kuna uwezekano wa
kuondoa vikwazo hivyo ili wafanye biashara zao kwa uhuru.
Wito huo umetolewa jana na Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mpato Tanzania
(TRA) Bw.Enosi Mjimba wakati wa Semina ya mafunzo ya elimu ya mlipa kodi kwa
mfanyabiashara semina ambayo ilifanyika Mpanda Mjini.
Alisema kuwa mfumo wa ulipaji kodi
ulioanzia Julai mosi mwak huu kwa mwaka wa fedha2016/2017 umeleta mabadiliko
katika sheria ya Kodi ya Mapato,Kodi ya ongezeko la thamani,Sheria ya mamalaka
ya Mapato Tanzania,Sheria ya usimamizi wa kodi,Sheria ya usimamizi wa Vyombo
vya moto na Sheria ya VETA.
Kwa upande wake Afisa Huduma na Elimu
kwa Mlipa kodi mkoa wa Rukwa na Katavi Bw.Philipo Eliaminy amewataka wenye
tabia ya kuuziana vyombo vya usafiri kama pikipiki mitaani wafike katika Ofisi
za Mamlaka ya Mapato Tanzania na kubadili majina ya usajili ili kuepuka gharama
zinazotokana na kulipa madeni aliyokuwa akidaiwa aliyemuuzia kwa kuwa jina la
mdaiwa litaonekana la mmiliki wa awali.
Nao baadhi ya wafanyabiashara
wakiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiasahara Tanzania Tawi la Katavi
Bw.Aman Mahellah na Mwenyekiti wa Wenye viwanda,kilimo na Biasahara Wilayani
Mpanda Bw.Shabir Dalla mawesema kuwa miongoni mwa changamoto zinazotakiwa
kufanyiwa kazi haraka na TRA ni pamoja na kuimarisha mitandao ya Mashine za
EFDs,kutoa elimu mara kwa mara ya mlipa kodi kwa mfanyabiashara na kuwakilisha
matatizo ya wafanyabiasahara ngazi za juu ili yafanyiwe kazi haraka.
Katika Shilingi Trilioni 29.5 za
makadirio ya serikali katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 zinazotarajiwa
kutumiwa na serikali katika uendelezaji wa shghuli mbalimbali,Mamalaka ya
Mapato Tanzania TRA imepangiwa kukusanyanya Shilingi Trilioni 15.1.
Wafanyabiasahara wapatao 100
walishiriki katika semina ya mafunzo ya elimu ya mlipa kodi ambapo hii ni
semina ya kwanza kufanyika Mkoani Katavi Tangu Mwaka wa fedha 2016/2017 uanze
mwezi Julai mwaka huu kuhusu mfumo mpya wa elimu kwa mlipa kodi unaowahusisha
wafanyabiasahara.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Habarika Zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments