WAZIRI MKUU WA INDIA KUWASILI LEO TANZANIA KUANZA ZIARA,SEKTA ZA VIWANDA,MAJI,ELIMU,SAYANSI NA TECHNOLOJIA KUPEWA KIPAUMBELE
WAZIRI Mkuu wa India, Narendra Modi anawasili leo nchini kwa
ajili ya ziara ya kitaifa ya siku mbili kwa lengo la kudumisha ushirikiano
katika sekta mbalimbali kati ya nchi hizo mbili.
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi |
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam,
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Augustine Mahiga
alisema Modi atatumia fursa hiyo kukuza uhusiano wa kihistoria baina ya nchi
hizi mbili pamoja na kufungua maeneo mapya ya ushirikiano wa kiuchumi.
Alisema Modi atakutana na Rais John Magufuli Ikulu na kufanya
naye mazungumzo.
Akiwa hapa nchini atasaini mikataba mbalimbali ya ushirikiano
kati ya sekta za viwanda, maji, elimu, sayansi na teknolojia na baadaye
kuzungumza na waandishi wa habari.
Aidha Dk Mahiga alisema Modi pia atazungumza na jumuiya ya
wafanyabiashara wakubwa wa India ambao baadhi yao wameshaonesha nia ya kuwekeza
katika sekta ya ujenzi wa viwanda vya kutengeneza chuma, saruji, dawa ya
binadamu na maji ya matunda.
Kongamano hilo litakalowakutanisha wafanyabiashara mbalimbali
hapa nchini linatarajia kufanyika katika ukumbi wa Benki Kuu (BoT) na Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi huku Waziri wa mambo ya nje wa
Tanzania Dk Augustine Mahiga akiwataka wafanyabiasha wa Tanzania kutumia fursa
hii kushiriki ipasavyo ili waweze kukutana na wafanyabiashara wenzao.
Endelea
kuhabarika na P5 TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni tuma
kupitia p5tanzania@gmail.com
Comments