MWENGE WA UHURU KUWASILI KESHO MKOANI KATAVI,WANAKATAVI WAASWA KUDUMISHA AMANI
WANANCHI mkoani Katavi wametakiwa kudumisha amani na utulivu
katika kipindi hiki ambacho wanatarajia
kupokea mwenge wa uhuru.
Rai hiyo imetolewa
na Kaimu kamanda mkoa wa Katavi
Focas Malengo wakati akizungumzia kuhusu mandalizi ya upokezi wa mwenge
wa uhuru unaotarajia kuwasili julai 10 mwaka huu.
Ameongeza kusema kuwa mwenge huo ukiwa mkoani hapa unatarajia kuzindua miradi mbalimbali
ya maendeleo.
Aidha ameeleza kuwa kilele cha mbio za mwenge kinatarajiwa
kuwa julai 14 katika mkoa huu ambapo utaelekea mkoani Kigoma.
Mwenge wa uhuru ulizinduliwa Mkoani Morogoro Aprili 8 mwaka
huu na Makamu wa Rais wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan ambapo kilele chake
kitahitimishwa Oktoba 14 Mkoani Simiyu.
Kauli mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka huu ni ‘’Vijana ni nguvu kazi ya
taifa,Washirikishwe na kuwezeshwa’’
Comments