WAKAZI KATAVI WAENDELEA KUCHAMBUA UTEUZI WAKURUGENZI WAPYA WAWASHAURI WAKURUGENZI KUTEKELEZA KAULI MBIU YA ‘’HAPA KAZI TU’’ IPASAVYO
Wakazi
Mkoani Katavi wamesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania uteuzi wa
wakurugenzi alioufanya Julai 7 mwaka huu ni mzuri ikiwa walioteuliwa watafanya
kazi kwa kuzingatia kiapo cha maadili na utumishi wa umma wanachoapa kabla ya
kuanza kazi.
Rais Dkt.John Pombe Magufuli |
Wamesema
kuwa wakurugenzi walioteuliwa katika
Halmashauri zilizopo Mkoani Katavi wamewsahauri kusimamia kwa misingi ya haki ili
kuleta maendeleo ya wananchi.
Miongoni
mwa wananchi ambao wametoa maoni ni pamoja na Askofu wa makanisa ya New Harvest
Tanzania Askofu Laban Ndimubenya,baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa
vilivyopo Mkoani Katavi sanjari na wananchi wa kawaida.
Maoni
hayo yametolewa ikiwa ni siku chache baada ya kuteuliwa na Rais John Pombe
Magufuli Julai 7 mwaka huu ambapo wanatarajia kuapishwa siku ya Jumatatu Julai
12 mwaka huu.
Halmshauri
za Mkoa wa Katavi zilizopata wakurugenzi wake ni pamoja na
1.Mlele
DC
- Alex Revocatus
Kagunze
2.Mpimbwe
DC
- Erasto Nehemia
Kiwale
3.Mpanda
DC
- Ngalinda Hawamu
Ahmada
4.Mpanda
Manispaa
- Michael Francis
Nzyungu
5.Nsimbo
DC
- Joachim Jimmy
Nchunda
Uteuzi
wa wakurugenzi unahusisha halmashauri za majiji 5, Manispaa 21, Miji 22 na
Wilaya (DC) 137 za Tanzania Bara.
Kati
ya wakurugenzi wote 185 walioteuliwa,65 waliteuliwa kutoka orodha ya
wakurugenzi wa zamani waliokuwa katika serikali ya awamu ya nne iliyokuwa
ikiongozwa na Rais msitaafu wa awamu ya nne Mh.Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete
huku wakurugenzi wakiwa wapya 120 wengi wao wakiwa vijana.
Wakurugenzi wameteuliwa siku chache
baada ya uteuzi wa wakuu wa Wilaya kuteuliwa Juni 26 mwaka huu ambapo wakuu wa
wilaya katika Wilaya za Mkoa wa Katavi ni pamoja na
1. Mlele
Rachiel Stephano
Kasanda
2. Mpanda
Lilian Charles
Matinga
3. Tanganyika
Saleh Mbwana
Mhando
Wakuu
hawa wa Wilaya tayari wamekwishaapishwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi mpya wa Mkoa
wa Katavi Meja Jeneral Raphael Mugoya Mhuga
Mwandishi:Issack
Gerald Bathromeo
Mhariri:Issack Gerald
Bathromeo
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments