NEC YAKABIDHI RIPOTI YA TAARIFA YA UCHAGUZI KWA SERIKALI YA MKOA WA KATAVI
Tume ya taifa ya uchaguzi NEC imeikabidhi
serikali ya Mkoa wa Katavi ripoti ya taarifa ya uchaguzi wa udiwani,ubunge na
urais uliofanyia mwaka jana Oktoba 25.
Akikabidhi ripoti hiyo katika Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi mbele ya waandishi wa habari,Afisa wa tume ya
uchaguzi Taifa Bw.Peter Mwezi amesema,nakala za ripoti hiyo zitasambazwa katika
ofisi zote za serikali zikiwemo Ofisi tatu za wakuu wa Wilaya waliopo mkoani
Katavi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Meja Mstaafu Jeneral Raphael Mugoya Muhuga pamoja na kuipongeza tume kwa
kukamilisha uandaaji wa taarifa ya uchaguzi na kusimamia uchaguzi kwa amani na
utulivu,amesema ripoti hiyo inatakiwa kusomwa na kubaini maudhui yake.
Katika makabidhiano hayo mbali na
kuhudhuriwa na waandishi wa habari pia yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa
ngazi ya mkoa akiwemo Katibu tawala wa Mkoa wa Katavi Kamishna Paul Chagonja na
kaimu katibu tawala Salumu Shilingi.
Naye Mratibu wa uchaguzi Mkuu wa udiwani,ubunge
na Urais Mkoani Katavi uliofanyika Oktoba 25 mwaka 2015 ambaye pia ni kaimu
katibu tawala mkoani Katavi Bw.Salumu Shilingi,akizungumzia kuhusu mwongozo wa
sasa wa makabidhiano ya ripoti ya taarifa ya uchaguzi,pamoja na mambo mengine amesema
kutokana na umuhimu wa nafasi ya vyombo vya habari katika jamii,makabidhiano ya
taaifa kama hiyo yanatakiwa yafanyike mbele ya waandishi wa habari kama ambavyo
imefanyika.
Juni
23 mwaka huu,tume ya taifa ya uchaguzi NEC chini ya Mwenyekiti wake Jaji mstaafu
Damian Lubuva,ilimkabidhi ripoti ya taarifa ya uchaguzi huo Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri:Issack Gerald
Bathromeo
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments