CCM ANAYOKABIDHIWA MAGUFULI ILIANZA HIVI
LEO Julai
23,Rais wa awamu ya Tano wa Tanzania Rais Dkt.John Pombe Magufuli anatarajia
kupokea uenyekiti wa kukiongoza Chama cha Mapinduzi CCM)
Historia
ya Chama
CCM
ilizaliwa tarehe 5 Februari 1977 baada ya kuungana kwa
vyama vya Tanganyika African National Union
(TANU) kilichokuwa kikitawala Tanzania Bara na Afro-Shirazi Party (ASP) kilichokuwa chama
tawala cha Zanzibar
wakati huo. Chama cha TANU kilikuwa kikiongozwa na Mwalimu
Nyerere na Afro-Shiraz Party kilikuwa chini ya Amaan Karume.
Itikadi
Kwa
miaka mingi CCM ilikuwa ikifuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Itikadi
hii ilipewa nguvu za kisera mwaka 1967 lilipotangazwa Azimio la
Arusha.
Kutokana
na azimio
hilo uchumi
uliwekwa mikononi mwa umma. Itikadi hiyo pia ilisisitiza umuhimu
wa kuishi pamoja hasa katika vijiji vya Ujamaa.
Uchaguzi
CCM
imekuwa ikishinda chaguzi za Urais toka mfumo wa vyama vingi
uliporejeshwa nchini Tanzania.
Chama
hicho kimekuwa pia kikipata idadi kubwa ya wabunge wa Bunge la Muungano na Baraza la Wawakilishi,
ingawa vyama vya upinzani vilitoa
malalamiko kuhusu utekelezaji wa haki na uchakachuaji wa kura.
Chaguzi
za vyama vingi Tanzania baada ya kurejeshwa kwa mfumo huo zilifanyika mwaka 1995, 2000, 2005 na 2010 na viongozi walioweza
kuwa washindi kakati chama hicho ni kama wafuatao: Benjamin
Mkapa na Jakaya Mrisho Kikwete. Hawa ndio viongozi
waliongoza nchi kipindi cha miaka ishirini.
Katika
historia ya CCM kumekuwa na wenyeviti wanne:
1.Julius Nyerere, 1977 - 1990,
2.Ali Hassan Mwinyi 1990 - 1996
3.Benjamin Mkapa 1995 - 2005,
4.Jakaya Kikwete 2006 - hadi sasa
5.(…………….
Endelea kuelimika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments