KATAVI YAADHIMISHA SIKU YA MTOTO AFRIKA,NDANI YA MIEZI 6 WATOTO ZAIDI YA 30 WAFANYIWA UKATIRI KATAVI
Mkoa wa Katavi umeadhimisha maadhimisho ya siku ya mtoto wa
afrika ambapo maadhimisho hayo yamefanyika
katika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili.
Watoto waishio katika mazingira magumu na walemavu
wakizungumza katika maadhimisho hayo,wameiomba jamii kupinga ukatili wa kijinsia dhidi yao kwani wanaathirika kisaikolojia na
kudidimiza ndoto zao .
Akisoma risala mbele ya mgeni rasimi katibu wa baraza la watoto wenye ulemavu mkoani
Katavi Bw George Charles amezitaja
baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa vitendo
vya ulawiti,ubakaji ,ukosefu wa miundombinu
rafiki kwa walemavu mashuleni pamoja na mitazamo hasi juu ya watoto
wenye ulemavu.
Kwa upande
msemaji wa dawati la jinsia na watoto katika kituo cha polisi mpanda
H 311 DC Emanueli Lindege amekiri
kuwepo kwa matukio ya ulawiti na ubakaji kwa watoto ambapo kuanzia mwezi
January hadi juni kumeripotiwa na matukio ya ubakaji wa watoto zaidi ya 30.
Naye mgeni rasimi Bi.Josephina Chilongozi ambaye ni
mwanasheria na mwanaharakati wa haki za binadamu ameiomba serikali kuweka mazingira rafiki kwa
watoto waishio katika mazigira magumu na walemavu ambapo pia amewaasa
watoto kutoa taarifa kwa wazazi wao
wanapokutana na vitendo vya kikatili.
Maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi alikuwa waziri wa
maendeleo ya jamii jinsia na watoto Ummy Mwalimu.
Siku ya mtoto wa
afrika iliidhinishwa mwaka 1991 juni
16 ili
kuwaenzi watoto wenzao waliofariki kwa kupigwa risasi huko Soweto sauth
afrika mauaji hayo yakiwa yametokea mwaka 1979 kwakipinga ubaguzi wa rangi.
Maadhimisho haya ya mwaka huu yametumia kauli mbiu isemayo ‘’ubakaji na ulawiti wa watoto wadogo
unaepukika chukua hatua kumlinda mtoto.’’
Mwandishi :Issack
Gerald Bathromeo
Mhariri : Issack
Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments