JERA MIEZI 6 MPANDA AKITUHUMIWA KUJIPATIA FEDHA KWA UDANGANYIFU
Mahakama ya mwanzo mjini mpanda
imemhukumu mtu mmoja kwenda jera miezi sita au kulipa faini ya shilingi laki
mbili kwa kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
Akisoma hukumu hiyo hakimu
mkazi Mh.Ramadhani Mkumbi
amemtaja mshitakiwa kuwa ni Joseph
Lukasi mkazi wa Nsemluwa manispaa ya
Mpanda
Amsema kuwa mshitakiwa huyo alitenda
kosa hilo mnamo Juni 20 mwaka huu
maeneo ya Mpanda hoteli na
kujipatia kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni tatu
fedha ya Bw.felix Makombe mkazi
wa majengo ambapo alidai kuwa alichukua fedha hiyo kwa lengo la kumununulia
gunia 70 za mpunga lakini alitokomea na fedha hiyo pasipojulikana kitendo
ambacho ni kinyume na sheria za nchi.
Kufatia hatua hiyo mahakama
imemhukumu mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia kama hiyo.
Wakati huo huo mtu mwingine
amefikishwa mahakamani hapo kwa kosa la wizi.
Akisoma shitaka hilo mwendesha mashitaka wa jeshi la police PCL mtei
mbele ya hakimu mwandamizi David
Mbembela, amemtaja mshitakiwa kuwa ni Husseni Omari(12) mkazi wa Nsemluwa.
Amesema kuwa mnamo Mei 9 mwaka huu maeneo
ya Kichangani tarafa ya kashaulili,mshitakiwa aliiba godoro moja futi 5 kwa 6
aina ya komfy,shuka mbili zenye thamani
ya shilingi elfuThelathini na pesa tasilimu Laki laki moja na elfu sitini vyote vikiwa na thamani ya shilingi Laki tatu na elfu
sitini .
Hata hivyo mshitakiwa amekana shitaka
hilo na yupo nje kwa dhamana mpaka hapo kesi itakapotajwa tena Juni 30 mwaka huu kwa
ajili ya kusikilizwa.
Mwandishi :Ester
Lameck
Mhariri : Issack
Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments