AHUKUMIWA KIFUNGO CHA NJE MIEZI 6 KWA UBADHIRIFU WA FEDHA
Mahakama ya mwanzo mjini Mpanda
imemhukumu mtu mmoja kifungo cha nje miezi sita kwa kosa la matumizi mabaya ya
madaraka kwa kutumia fedha bila kufuata utaratibu wa ofisi.
Akisoma hukumu hiyo,hakimu mkazi
Mh.Sylivester Makombe,amemtaja mshtakiwa kuwa ni Enjoy Juniour(21)mkazi wa
Makanyagio,ambaye anadaiwa kutenda kosa hilo mnamo Mei mosi mwak huu wakati akitoa huduma katika
banda la Tigo-Pesa Mpanda Mjini.
Mh.Makombeamesema Bi.Enjoy alitumia
zaidi ya Shilingi milioni mbili kwa matumizi yasiyoeleweka ambapo kwa upande
wake mtuhumiwa amekiri kutenda kosa hilo mara baada yak up[ewa nafasi ya
kujitetea na ameomba kupunguziwa adhabu.
Hata hivyo mahakama imekubali
kumpunguzia adhabu ambapo pia imesema itaendelea kutoa adhabu kali kwa watu
wenye tabia kama hiyo ili iwe fundisho kwa wengine.
Wakati huo huo mtu mmoja
aliyefahamika kwa jina la Mgira Magembe(27) mkazi wa Mpanda Hotel amefikishwa
katika mahakama ya mwanzo kwa kosa la wizi wa baiskeli ina ya Sports yenye
thamani ya shilingi laki moja na nusu iliyokuwa imekodiwa na Mariam Willium
mkazi wa Kigambo.
Mwendesha mashtaka wa Jeshi la Polisi
Wilayani PC Mtei amesema kuwa tukio hilo limetokea leo Juni Mosi majira ya saa
12 asubuhi,katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda.
Hata hivyo mshtakiwa amekana kutenda
kosa hilo ambapo ameiambia mahakama kuwa baiskeli hiyo ameichukua kwa maelekezo
ya rafiki akijua kuwa ndiye mmiliki.
Mshtakiwa amepelekwa mahabusu baadaya
kukosa kukidhi vigezo vya dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 15 mwaka
huu kwa ajili ya kusikiliza maelezo ya mlalamikaji.
Mwandishi:Issack Gerald Bathromeo
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments