WAENDESHA PIKIPIKI(BODABODA) WILAYANI MPANDA WAIOMBA SERIKALI KUWAFUNGIA MTAMBO WA KUKATIA LESENI.



WAENDESHA pikipiki maarufu kama bodaboda wilaya ya Mpanda mkoani Katavi  wameiomba serikali kuwafungia mtambo wa kukatia lesini.

Hayo yamebainishwa jana Aprili 22,2016 katika kikao maalum kilicho shirikisha viongozi waandamizi kutoka jeshi la Polisi ambapo wamelitaja suala la kukosekana kwa mtambo huo kuwa changamoto kubwa inayo wakabili kwa sasa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha  waendesha bodaboda wilaya ya Mpanda  Bw.Stephano Asalile ameviomba vyombo vya usalama barabarani kuendelea kuto elimu zaidi
Kaimu kamanda mkoa wa Katavi Damas Nyanda  ameahidi kuzifanyia  kazi chanaga moto mbali mbali zinazo wakabili  madereva hao na kuwataka kutii sheria bila shuruti.
Naye Mkuu wa kituo cha polisi wilaya ya mpanda Bw.Zeno Malesa ametoa rai kwa watu waliokamatwa kwa makosa mbalimbali kuhusu pikipiki zao kufika kituoni ili kupatiwa pikipiki hizo.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA