RAIA WAPYA KATUMBA NA MISHAMO WATAKIWA KUTOJIHUSISHA NA VITENDO VYA UHARIFU.
Raia wapya waishio makazi mapya ya
Katumba na Mishamo wametakiwa kutojihusisha na vitendo vya uharifu na badala
yake wametakiwa kufuata sheria za nchi.
Kauli hiyo imetolewa na mwakilishi wa
shirika la kuhudumia wakimbizi duniani hapa nchi Tanzania Bi.Chansa Kapaya
wakati wa makabidhiano ya vyumba vine vya madarasa,nyumba moja ya mwalimu
katika shule ya sekondari Mazwe na bweni la wanafunzi katika shule ya Sekondari
Mishamo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mazwe Mwl.
Oswadi Sabasi Masawe anaona kwa upande wake nyumba na madarasa ni mkombozi kwa
walimu na wanafunzi.
Shule ya Sekondari Mazwe ina
wanafunzi 189 wa kidato cha kwanza kati ya 250 wanaotakiwa kuwepo shuleni hapo.
Comments