TAKUKURU YATOA TAKWIMU YA KESI NA MALALAMIKO ILIYOYAPOKEA MWEZI JANUARI HADI MACHI 2016,TAMISEMI WAIBUKA KIDEDEA
Na.Issack Gerald-Katavi
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa
TAKUKURU Mkoani Katavi imesema kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Machi mwaka
huu imepokea malalamiko 22 ya vitendo vya Rushwa.
Takwimu hiyo imetolewa na Mkuu wa
Takukuru Mkoani Katavi Bw .John Minyenya wakati akizungumza na waandishi wa
habari Ofisini kwake.
Bw.Minyenya amesema kuwa taasisi
zinazoongoza kwa kuhusishwa na malalamiko
ya vitendo vya Rushwa kwa kipindi hicho ni Tawala za mikoa na serikali za
Mitaa(TAMISEMI) ambapo Halmashauri zina jumla ya malalamiko 14,Jeshi la Polisi malalamiko 4,idara ya mahakama lalamiko 1,idara ya afya 1,Sekta binafsi 1 na
mashirika ya umma 1.
Aidha amesema,Takukuru Mkoani Katavi
ina Jumla ya ya kesi 5 zinazoendelea mahakamani zikiwa katika hatua mbalimbali
huku kesi 2 zilizofunguliwa katika
kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2016 ambazo ni CC.12/2016 inayomhusu
Bi.Catherine Isack Kipeta ambaye ni Afisa mtendaji wa mtaa wa Kawajense
anayeshitakiwa kwa kuomba Rushwa ya shilingi Elfu thelathini(30,000/=) kinyume
na kifungu cha 15 ya sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa Na.11/2007.
Amesema kuwa Mtendaji huyo alipokea
hiyo fedha kutoka kwa mfanyabiashara ambaye alifungua biasahara siku ya
jumamosi ambayo ni siku ya usafi.
Kesi nyingine ameitaja kuwa
inamhusisha PC Peter Exavery Kashuta askari wa kituo kidogo cha polisi Mwese
aliyepokea Rushwa ya Shilingi laki moja (100,000) kati ya laki saba (700,000)alizokuwa
akihitaji ambapo alipokea rushwa hiyo ili kufuta kesi ya mwananchi mmoja
aliyekuwa akituhumiwa kumjeruhi mwanaye baada ya kupiga na jiwekichwani.
Watakti huo huo Takukuru imetoa wito
kwa wakazi Mkoani Katavi kujitokeza na kuunga mkono juhudi za TAKUKURU ili
kuongeza mapambano dhidi ya vitendo vya Rushwa.
Comments