MGANGA MKUU HOSPITALI YA WILAYA YA MPANDA AKANUSHA WAGONJWA NA WAJAWAZITO KULAZIMISHWA KUPIMWA VVU BILA HIARI.
Na.Issack Gerald-Mpanda
HOSPITALI YA WILAYA Mganga mkuu
Hospitali ya Wilaya ya MpandaDk.Naibu Mkongwa,amekanusha taarifazilizosambaa
kuwa wanawalazimisha wagonjwa kupima Virusi vya Ukimwi wanapokuwa wamefika
hospitalini hapo kutibiwa.
Dk.Naibu Mkongwa amekanusha hali hiyo
wakati akijibu hoja za balaza la madiwani kupitia kikao chake cha tatu ambacho
kimefanyika jana Mjini Mpanda.
Amesema wanapimwa bila hiari na kwa
amri ya mahakama ni pamoja pamoja na watuhumiwa wa ubakaji na mwathririwa wa
ubakaji pia wanawekewa viungo bandia vikiwemo figo moyo.
Kwa upande mwingine,Kituo cha Afya
cha Mwese ni miongoni mwa vituo vya afya vilivyopo katika Halmashauri hiyo
ambapo kituo kicho kinakabiliwa na tatizo la kutokuwa na maji,uchakavu wa
mashuka na ukosefu wa dawa ambapo kwa mjibu wa diwani wa Kata ya Mwese,kituo
hicho kimekuwa kikipata chupa moja ya vidonge(Tembe).
Kwa mjibu wa wakuu wa idara ya Afya
wa Halmshauri wakijibu hoja za balaza la madiwani,wamesema kuwa milioni 720
zimetengwa kwa ajili ya kunusuru hali ya kituo hicho cha afya.
Wakati huo huo licha ya kuwepo mafanikio
ya maendeleo katika baadhi ya kata mbalimbal zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya
Mpanda,kata hizo zimeonekana kuwa na changamoto katika sekta ya
afya,miundombinu ya barabara na elimu.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Hamad Mapengo na Mkurugenzi mtendaji Estomihn
Chang’a wamewashauri madiwani
kuwashirikisha wananchi katika vijiji na kata zao katika utatuzi wa baadhi ya
changamoto za maendeleo zilizo ndani ya uwezo wao
Comments