SILAHA 11 KATAVI ZASALIMISHWA WAKATI WA ZOEZI LA UHAKIKI,ZAIDI YA ASILIMIA 60 HAZIJAHAKIKIWA
Na.Issack Gerald-Katavi
Jumla ya silaha 11 kati ya 193
zinazomilikiwa kisheria Mkoani Katavi zimesalimishwa huku silaha 76 kati ya
hizo 193 zikiwa zimehakikiwa kuanzia Machi 21 hadi Aprili mwaka huu.
Jeshi la Polisi limekuwa na utaratibu
wa kutoa takwimu mbalimbali kulingana na matukio yanayoendelea kujitokeza.
Machi 21 mwaka huu,Jeshi la Polisi
Mkoani Katavi lilitoa wito kwa wanaomiliki silaha kufika katika vituo vya
polisi,Ofisi za serikali za mitaa kuhakiki au kusalimisha silaha lengo likiwa
kudhibiti uharifu.
Kutokana na mikakati hiyo,Jumla ya
silaha 11 kati ya 193 zinazomilikiwa kisheria Mkoani Katavi zimesalimishwa huku
silaha 76 kati ya hizo 193 zikiwa zimehakikiwa kuanzia Machi 21 hadi Aprili
mwaka huu.
Taarifa hiyo ya uhakiki imetoleewa Aprili
15,2016 na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi SSP Damas Nyanda wakati
akizungumza na waandishi wa habari Ofisini Kwake,kuhusu zoezi la uhakiki na
usalimishaji wa silaha zinazomilikiwa
kinyume cha sheria za nchi.
Wakati huo huo zikiwa zimesalia
takribani siku 32 kabla ya zoezi la uhakiki kufikia ukomo,pamoja na mambo
mengine kamanda Nyanda ametoa onyo kwa watu wanaomiliki silaha ikiwa ni kutoziazimisha
kwa watu wengine au makampuni na badala yake wazitumie kwa mujibu wa sheria na
taratibu za nchi.
Kwa nyakati tofauti tofauti Inspekta
Jenerali wa jeshi la Polisi Tanzania IGP Ernest Mangu amekuwa akisikika
akiwaagiza makamanda wa polisi mikoa yote ya Tanzania hususani Tanzania bara
kusimamia zoezi la uhakiki.
Katika hatua nyingine SSP Nyanda
amesema katika silaha 76 zilizohakikiwa Shot Gun ni 48 sawa na
39%,Pistol(Bastola) 16 sawa na 40%,Rifle 12 sawa na 40 huku silaha
zisizohakikiwa 61% kwa Shot Gun,60% kwa Bastola,60% kwa Rifle ambapo kwa ujumla
ni sawa na 39.3% kwa silaha zilizohakikiwa na 60.6% kwa silaha ambazo
hazijahakikiwa.
Katika mkoa wa Katavi silaha
zinazomilikiwa kihalali ni Shot Gun 123,Bastola 40,Rifle 30 wakati ikiwa hakuna
gobole hata moja.
Zoezi la uhakiki na usalimishaji wa
silaha linatarajia kuhitimishwa ifikapo Mei 20 mwaka huu.
Agizo la Uhakiki na usalimishaji wa
silaha kwa mara ya kwanza mkoani Katavi kwa mwaka 2016 lilianza Januari 6.
Endelea kufuatilia P5 TANZANIA
MEDIA, Kwa maoni au ushauri p5tanzania@gmail.com
Comments