MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO MTEGONI,APEWA SIKU SABA KUCHUNGUZA MHANDISI MWENYE DHARAU NA JEURI KWA VIONGOZJI WA SERIKALINI NA UBINAFISI WA MATUMIZI YA GARI,UHAKIKI WATUMISHI HEWA NALO LAENDELEA KUMTESA MKURUGENZI
Na.Issack Gerald-Nsimbo
Mkurugenzi
Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bw.michael zyungu amepewa siku 7
kuchunguza kazi ya mhandisi aliyetajwa kwa jina mojala Mh. Mbotu anayetuhumiwa
kudharau na kuonesha jeuri kwa viongozi wa ngazi za juu serikalini pamoja na ubinafsi
katika kutumia mali za Halmashauri likiwemo gari la halmashauri hiyo.
Agizo hilo
limetolewa Aprili 15,2016 na mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mh.Raphael Kalinga katika kikao cha madiwani
kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo.
Aidha
ameongeza kuwa katika Halmshauri hiyo kuna watumishi hewa katika idara ya elimu ya msingi na sekondari ambao
wanaendelea kulipwa mishara ambapo pia Mh.Kalinga ameuagiza uongozi wa
Halmashauri kupata takwimu ya watumishi hao wanaoendelea kulipwa mishahara
ndani ya hizo siku 7 ili hatua za kisheria zichukuliwe.
Katika hatua
nyingine,watendaji wa serikali wametakiwa kutoa ushirikiano kwa
madiwani ili kutatua changamoto za wananchi huku akisema kuwa watendaji
wasiowajibika ipasavyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao
Halikadhalika
Kalinga ametoa wito kwa viongozi wa umma kufanya kazi kwa weledi ikiwa ni
pamoja na kusimamia mapato ya ndani ya halmashauri husika ikizingatiwa kuwa Wiki
iliyopita serikali ilitangaza kuzifuta
halmashauri zote zitakazo shindwa kukusanya mapato ya ndani kwa kiwango cha 80%
.
Kwa upande
wake Mkuu wa wilaya ya mlele Kanali Mstaafu Issa Sulemani Njiku amewataka
viongozi wa Halmshauri kuhakikisha wanasimamia ipasavyo zoezi la kuwatambua
watumishi hewa katika maeneo mbalimbali wakiwemo waliopo katika idara ya
afya,elimu pamoja na kilimo
Endelea
kufuatilia P5 TANZANIA MEDIA,Kwa maoni au ushauri p5tanzania@gmail.com
Comments