RC KATAVI AFANYA ZIARA HOSPITALI YA WILAYA MPANDA,ASEMA SERIKALI IMETENGA BIL.2 KUTUMIKA UJENZI HOSPITALI YA MKOA KUPUNGUZA MSONGAMANO WA WAGONJWA.
Na.Vumilia Abel-Katavi
MKUU
wa mkoa Meja Jeneral Raphael Muhuga amefanya ziara ya kuitembelea hospitali ya wilaya
ya Mpanda kwa lengo la kutazama changamoto zinazoikabili hospitali hiyo.
Akizungumza
jana na wahudumu katika hospitali hiyo mkuu huyo wa mkoa amesema,moja ya
changamoto alizozibaini ni uhaba wa dawa, Madaktari,wauguzi,uchakavu wa majengo.
Jeneral
Muhuga amesema serikali imetenga kiasi
cha shilingi BIL.2 kwa ajili ya ujenzi wa hospital ya mkoa ili kuepusha
msongamano unaoweza kujitokeza ikiwa ni pamoja na kuondoa tatizo la wagonjwa
wawili kulala kitanda kimoja.
Aidha
ametoa rai kwa wananchi wanaojichukulia sheria mkononi kwa kuwapiga madaktali wanaotoa huduma kuacha mara moja
kwani kwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria ya nchi.
Wakati
huo huo Mkuu wa Mkoa ametembelea chuo cha afya ambacho kina lengo la kutoa mafunzo kwa wanganga
wasaidizi ili kutatua tatizo la upungufu wa wanganga.
Naye
Mhandisi anayejenga chuo hicho amemhakikishia Mkuu wa mkoa kumaliza ujenzi huo ifikapo
mwezi juni mwaka huu.
Kwa
upande wake kaimu mganga mkuu wa hospitali ya wilaya Bw.Benard Kamande amesema Hospitali
hiyo inakabiliwa na ufinyu wa bajeti kuhudumia mkoa mzima wa Katavi,ubovu wa
magari ya kubeba wagonjwai pamoja na upungufu wa wahudumu 157.
Comments