AJALI ZITOKANAZO NA VYOMBO VYA MOTO KATAVI ZAPUNGUA.
Na.Issack
Gerald-Katavi
KIKOSI
cha usalama barabani Mkoani katavi
kimesema kimefanikiwa kupunguza ajali za
barabani kwa kutumia kifaa maalum cha kupima mwendo kasi.
Kauli
hiyo imetolewa na mkuu wa usalama barabani Mkoani Katavi Bw John Mfinanga wakati akitoa takwimu za ajali
barabarani kuanzia mwezi January
hadi April mwaka 2016.
Hata
hivyo amesema kuwa kifaa hicho
kina uwezo wa kupima madereva
ambao wamelewa wakati wakiwa barabarani.
Aidha
kikosi hicho kimekuwa kinatoa elimu na kuwashauri watu wanaotumia kilevi kuacha kabisa wanapokuwa wanaendesha vyombo
vya moto.
Pia
ametoa wito kwa jamii kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pindi wanapoona dereva
anaendesha kwa mwendo kasi au akiwa na dalili za kutumia kilevi ili kulinda
usalama wa abiria.
Amesema kuwa katika kipindi hicho cha
miezi mitatu ni ajali nne ambazo zimetokea zikihusisha pikipiki huku katika
kipindi kilichopita ajali zilikuwa zaidi ya hapo.
Comments