MGOGORO WA ARDHI MTAA WA NSEMULWA MANISPAA YA MPANDA WAENDELEA KUTOKOTA,WANANCHI WAMWANGUKIA MKUU WA WILAYA
Wakazi wa mtaa wa Nsemulwa Kata ya
Nsemulwa Manispaa ya Mpanda,wamemwomba Mkuu wa Wilaya kumaliza tatizo la
upimaji waardhi katika mtaa huo ambalo limedumu kwa kipindi kirefu bila
kupatiwa ufumbuzi.
Wakazi wa Mtaa wa Nsemulwa kwa muda
mrefu sasa,wamekuwa wakihaha zaidi namna gani waishi kwa amani bila bughudha
yoyoye inayohusiana na migogoro ya ardhi inayolenga upimaji.
Kutokana na wakazi hao kupaza sauti
zao na wakati mwingine bila kusikilizwa kwa mjibu wa madai yao,hatimaye Ofisi
ya Mkuu wa Wilaya ikaamua kufika eneo la mgogoro kupata zaidi kero za wananchi
juu ya maeneo yao kwa njia ya kufanya mkutano wa hadhara.
Pamoja na mambo mengine wakazi hao wa
mtaa wa Nsemulwa wakamwomba Mkuu wa Wilaya kumaliza tatizo la upimaji wa ardhi
katika mtaa huo tatizo ambalo limedumu kwa kipindi kirefu bila kupatiwa
ufumbuzi.
Kupitia kikao cha hadhara kati ya
Uongozi wa Wilaya ya Mpanda na idara za ardhi Manispaa ya Mpanda ambacho
kimefanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Nsemulwa wananchi wakapewa fursa
ya kueleza madai yao.
Kutokana na baadhi ya wananchi
kueleza kutokuwa na uwezo wa kulipia gharama ya upiamji wa ardhi sanjari na
kupatiwa hati miliki,imemlazimu Mkuu wa iadara ya Ardhi,mpango mji na maliasili
Manispaa ya Mpanda Bw.Peter Makalipa kutoa ufafanuzi juu ya gharma ambapo
amesema kuwa punguzwa kwa gharama za upimaji na hati ya kiwanja litapelekwa
katika mamlaka husika ili lipitiwe upya kama ambavyo wananchi wameomba.
Kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya
Mpanda,Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Bw.Lauteri Kanoni amewataka
wananchi wenye malalamiko juu ya viwanja vyao kufika Ofisini ili madai yao
yashughulikiwe kwa wakati na kwa mjibu wa sheria.
Kwa mjibu wa wananchi hao zaidi ya
800 wenye mgogoro wa ardhi katika mtaa wa Nsemulwa,mgogoro huo umedumu kwa
takribani miaka mitano mpaka sasa.
Comments