AFIKISHWA MAHAKAMANI MPANDA KWA MADAI YA KUUA BILA KUKUSUDIA
MTU Mmoja Mkazi wa Mji wa Zamani Katika Manispaa ya Mpanda
amefikikishwa Katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mjini Mpanda kwa Kosa la Kuua
bila Kukusudia.
Akisoma shitaka shitaka hilo mbele ya hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Mwanasheria wa
Serikali Bw,Lugano Mwasubira amesema mtuhumiwa anayefahamika kwa jina la
Priskus Michael alitenda kosa hilo mnamo tarehe 14 Aprili mwaka huu Katika eneo
hilo.
Mwasubira ameeileza Mahakama Kuwa mtuhumiwa alitenda Kosa
hilo kwa Kumuua Shukurani Salum Karongo ambapo Upelelezi unaendelea ilin
Kubaini chanzo cha Mauaji hayo.
Shitaka hilo limepangaiwa Kusikilizwa tena tarehe 11/5/2016
kwa Kuzingatia Kanuni na Sheria ambapo Mtuhumiwa amerudishwa Mahabusu Kusubiri
tarehe hiyo ya Kujibu Mashitaka dhidi yake.
Comments