MAHAKAMA YA WILAYA YA MPANDA YAFUTA HATI YA MASHTAKA YA WATU WAWLI KATI YA WATATU WALIOKUWA WAKITUHUMIWA KUIBA PIKIPIKI YENYE THAMANI YA SH.MIL.1.8
MAHAKAMA
ya mwanzo mjini mpanda imefuta hati ya mashta ya watu wawili kati ya watatu
waliokuwa wanakabiliwa na tuhuma za wizi wa pikipiki yenye thamani ya shingi
milioni moja na laki nane.
Uamuzi
huo wa mahakama umekuja mara baada ya mlalamikaji kuondoa shtaka hilo na kudai
ana mtambua mshtakiwa Bw Paul Willson (19)mkazi wa Nsemurwa kama mwizi wake na
si mtu mwingine
Akisikiliza
kesi hiyo hakimu mwandamizi David Mbembela amewataja washtakiwa ambao
wameondolewa katika shtaka hilo kuwa ni Bw Jackson Willson (17) na Thadeo
Nobert(19) wakiwa wote ni wakazi wa manispaa ya Mpanda.
Mbembela ameagiza jeshi la polisi kuandaa hati
ya mashtaka ikiwa na mtuhumiwa mmoja na
hatimaye ameahilisha shtaka hilo hadi litakapo tajwa tena april 21 mwaka huu.
Comments