KUMBUKUMBU YA MIAKA 32 KIFO CHA HAYATI EDWARD SOKOINE
Edward Moringe Sokoine (1938
- 12 Aprili
1984) alikuwa mwanasiasa kutoka nchi ya Tanzania.
Aliwahi kuwa Waziri Mkuu
mara mbili, tangu tarehe 13 Februari 1977 hadi 7 Novemba
1980, tena
tangu tarehe 24 Februari 1983 hadi kifo chake, alipofariki
kufuatana na ajali
ya gari.
Uongozi wake ulionekana kuwa wa mfano kwa jinsi alivyokuwa na
uadilifu na kufuatilia utendaji kazi huku
akikemea ulaji rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.
Sokoine alifariki kwa ajali ya gari wakati akitoka kwenye
kikao cha bunge
Dodoma
kuelekea Dar es Salaam. Wengi wanashuku ajali hiyo kuwa
ilipangwa.
Kifo chake kilileta majonzi makubwa kwa Watanzania wa kawaida
ambao walikuwa wanamtarajia kuwatetea wanyonge na kuinua hali ya maisha yao.
Chuo cha
Kilimo na Mifugo Morogoro kilipewa jina la "Chuo cha Kilimo cha
Sokoine" ambacho kwa sasa ni Chuo Kikuu cha Sokoine.
Comments