KUPATIKANA KWA SHIVYAWATA KATAVI MKOMBOZI KWA WENYE ULEMAVU
Na.Issack Gerald-Katavi
Kupatikana kwa uongozi wa Shirikisho
la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania SHIVYAWATA mkoani Katavi, kutaongeza
nguvu katika kutetea haki na kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye
ulemavu Mkoani hapa.
Maslahi au haki ya watu wenye ulemavu
kwa muda mrefu hapa Tanzania,yamekuwa yakitetewa na vyama vya watu wenye
ulemavu,wadau wa haki za binadamu wakati mwingine SHIVYAWATA linalojumuisha
umoja wa vyama hivyo .
Mwenyekiti wa Shivyawata Mkoani
Katavi Bw.Issack Mlela amesema kuwa,kabla ya kuunda shirikisho hilo,ilikuwa
vigumu kutetea haki za mlemavu kwani kila chama kilikuwa na utetezi wake binafsi
na hivyo kutokuwa na hoja ya nguvu ya pamoja.
Aidha mwenyekiti huyu amesema kuwa kupatikana
kwa uongozi wa Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania SHIVYAWATA
mkoani Katavi, kutaongeza nguvu katika kutetea haki na kutatua changamoto
zinazowakabili watu wenye ulemavu Mkoani hapa.
Aidha Bw.Mlela amewaomba watu wenye
uwezo wa kipato kusaidia shirikisho hilo kuanzisha miradi ya maendeleo ili
kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili zikiwemo kukosa Ofisi yao maalumu.
Uchaguzi wa viongozi wa shivyawata
Mkoani Katavi,ulifanyika mwezi Machi mwaka huu ukishirikisha vyama vitatu
vilivyopo Katavi kati ya vitano vilivyopo Tanzania vikiwemo TLB Chama cha
wasioona Tanzania na TAAS Chama cha wenye ualbino.
Pamoja na kubainisha changamoto
zinazowakabili pia Mlela anatoa wito kwa jamii yenye uwepo wa kipato.
Jumla ya viongozi sita ndiyo
wanaongoza Shirikisho la vyama vya watu wenye uelamavu SHIVYAWATA Mkoani Katavi
ambao ni Bw.Issack Mlela mwenyekiti
wa shirikisho hilo anayetoka katika chama cha wasioona TLB,Martha Iddy katibu Kutoka chama cha watu wenye ulemavu wa viungo CHAWATA,Prasido Kameme kutoka Chawata,Francisco Mazwazwa kutoka chama cha
wasioona,Ashura Shabaani kutoka Chama
cha wenye ualbino ,Rehema Maganga
kutoka chama cha wenye ualbino TAAS,Chama cha wenye mtindio wa ubongo na chama
cha wenye ulemavu wa kutosikia yaani viziwi.
‘’Ulemavu ni hali ya kuwa na hitilafu ya kudumu mwilini au akilini inayomzuia mtu kutekeleza shughuli zilizo kawaida katika maisha ya jamii’’ ambao haki zao husimamiwa na
sheria namba.9 ya mwaka 2010 ili waheshimike,wathaminiwe,walindwe na wapatiwe
haki zao za msingi ikiwemo elimu ,kupatiwa matibabu.
Taasisi ya Foundation For Civil
Society limekuwa likonekana kutoa semina mbalimbali kwa vyama vya watu wenye
ulemavu Mkoani Katavi ukiwemo Mkoa wa Katavi semina hizo zikilenga kutambua
haki za mwenye ulemavu,majukumu ya wenye ulemavu,jamii na viongozi wa
kiserikali.
Comments