JERA MWAKA MMOJA WILAYANI MPANDA KWA KUENDESHA UVUVI NDANI YA HIFADHI
Na.Vumilia
Abel-Mpanda
MAHAKAMA
ya Wilaya Mjini Mpanda imemuhukumu mtu mmoja mkazi wa Kakese kwenda jela mwaka mmoja kwa makosa mawili likiwemo la kujishughulisha
na uvuvu ndani ya hifadhi bila kibali.
Akitoa
hukumu hiyo,hakimu mkazi Orida Amworo amesema mnamo tarehe 31 mwezi agost 2015
majira ya saa 7 mchana mshitakiwa Donald
Nkwibi aliingia ndani ya hifadhi bila kibali pamoja na kufanya shughuli za
uvuvi mto Kantyentye .
Amworo
ameongeza kusema kuwa kosa la kwanza
kuingia ndani yahifadhi bila kibali mshitakiwa atatumikia kifungo cha miezi
sita jela na kosa la pili kuvua samaki kilo 30 aina ya kambale atatumikia
kifungo miezi sita.
Kwa
upande wake mshitakiwa amekili kosa na mahakama imemuhukumu kwenda jela.
Comments