WANNE WAKAMATWA NA MENO YA TEMBO KATAVI
Na.Issack Gerald-Mlele
Jeshi
la Polisi Mkoani Katavi linawashikilia watu 4 kwa tuhuma za kukutwa na vipande vitatu
vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu 11 vyenye thamani ya shilingi milioni 32,530,650/=ambayo ni sawa na tembo 01 aliyeuawa.
Kamanda
msaidizi wa Polisi Mkoani Katavi ACP Rashid Mohamed amewataja watuhumiwa hao kuwa ni
Frank Koroneli (25) Adela Alex (23) Moris ezron (34) na Sedekia Shadrack(38)
ambao ni wote wakazi wa kijiji cha Nduwi kata ya Katumba Wilayani Mlele.
ACP
Mohamed amesema kuwa,mnamo tarehe 05.03.2016 maeneo ya Msasani Kijiji cha Nduwi
Station Kata ya Katumba,Jeshi la Polisi likiwakatika katika ya doria walipata
taarifa toka kwa raia wema kuwa huko katika Kijiji cha Nduwi kuna wakazi wanajihusisha
na shughuli haramu za ujangili ambapo baada ya taarifa hiyo kupokelewa ndipo walipofuatilia
na kuweka mtego na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wakiwa na vielelezo hivyo huku
wakiwa wamevificha vipande hivyo kwenye kichaka.
Watuhumiwa
wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayowakabili mara baada
ya upelelezi kukamilika.
Hata hivyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi
ametoa wito kwa wananchi kutojihusisha na shughuli haramu za ujangiri na
biashara za nyara za serikali kwani ni
uhalibifu wa rasilimali za taifa letu hasa kwa manufaa ya vizazi vijavyo na
amesisitiza kuwa hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa kwa wale wote
wasiotii sheria pasipo kushurutishwa.
Comments