WANAWAKE WILAYANI MPANDA WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE KWA KUFANYA USAFI HOSIPTALINI
Na.Issack Gerald-Mpanda
WANAWAKE Mkoani Katavi,wameungana na wanawake wengine duniani
kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
Katika Wilaya ya Mpanda maadhimisho haya yamefanyika kwa
kufanya usafi katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda wakiongozwa na Mbunge wa
viti maalum mkoani katvi mh.Anna Lupemmbe ili kuwasidia wagonjwa ambao hawawezi
kufanya usafi.
Akizungumzia siku ya Wanawake duniani,mbunge huyo amesema
kuwa wanawake wamepiga hatua kubwa ya kimaendeleo kutokana na kutambua umuhimu
na nafasi yao katika jamii
Kwa upande wao wanawake wamefurahishwa na maadhimisho hayo yamewawezesha
kutafakari mchango wao katika kuisaidia jamii kimaendeleo
Siku ya wanawake duniani huadhimishwa kila mwaka ifikapo
machi 8 ambapo siku hii hutumika kujadili masula yanayowahusu wanawake ikiwa ni
pamoja na kujadili namna ya kutatua changamoto zinazowakabili.
Maadhimisho haya ya mara ya 41 tangu umoja wa mataifa
ulipotangaza rasmi kuanza maadhimisho haya mwaka 1975 yanaongozwa na kauli
mbiyu ya ‘’50-50 ifikapo 2030,tuongeze jitihada’’.
Comments