WANAWAKE KATAVI WASHAURIWA KUUNDA VIKUNDI ILI KUPATIWA MISAADA
Na.Meshack Ngumba-Katavi
Wanawake
Mkoani Katavi wameshauriwa Kujiunga na Vikundi ili kupata fursa ya Kupewa misaada itakayowasaidia Kujikwamua Kimaisha
kwa kuanzisha Miradi mbalimbali ya Maendeleo.
Ushauri
huo umetolewa na Mh,Taska Mbogo Mbunge Viti maalum Mkoa wa Katavi wakati wa
uzinduzi wa Vijiwe vya wanawake Katika kata za Uwanja wa ndege,Makanyagio na
Nsemulwa.
Katika
Uzinduzi huo Mh Mbogo ametoa Kiasi cha shilingi Milioni Moja na nusu kwa
vikundi vyote ili Kusaidia Uendeshaji wa Vikundi hivyo.
Wakizungumza
baada ya kupokea Msaada huo baadhi ya
akina mama waliohudhuria uzinduzi huo wamepongeza juhudi za Mbunge zinazolenga
kuwatoa wanawake katika kundi la watu tegemezi katika jamii.
Mkoani
Katavi kumekuwepo vikundi mbalimbali vya wanawake wanaojishughulisha na kazi
mablimbali ikiwemo utengenezaji wa sabuni,ufumaji wa vitambaa huku wengine
wakijishughulisha na ufugaji licha ya kuwa hakuna soko la uhakika wanakoweza
kuuzia bidhaa zao.
Comments