Na.Issack Gerald-Mlele
Jeshi la Polisi Wilayani Mlele Mkoani
Katavi linamshikilia Bw. Robert Nyakie(40) mkazi wa kijiji
na Kata ya kanoge barabara
ya tatu kwa tuhuma ya kukutwa na meno ya tembo kinyume na sheria.
|
ACP Rashid Mohamed,Kamanda Msaidizi wa Polisi Mkoani Katavi (PICHA NA.Issack Gerald)
|
|
Vipande vya meno ya tembo vikiwa Mezani(PICHA NA.Issack Gerald) |
|
Mtuhumiwa Bw.Robert Nyakie akiwa chini ya ulinzi (PICHA NA.Issack Gerald Machi 04) |
Kamanda Msaidizi wa Polisi Mkoani Katavi
ACP Rashid Mohamed amesema,mtuhumiwa ametenda kosa hilo mnamo Machi mosi mwaka
huu katika kijiji cha kanoge barabara ya kwanza.
Aidha,ACP Mohamed amesema,Bw.Nyakie akiwa na vipande
vinne vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu 11.50 ambavyo thamani
yake ni Shilingi milioni Ishirini na saba na laki saba na Elfu hamsini amabvyo
ni sawa na tembo mmoja aliyeuawa.
Mtuhumiwa
huyo aliyekuwa amevichimbia vipande hivyo nje karibu na ukuta wa nyumba yake,anatarajiwa
kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili mara baada ya upelelezi
kukamilika.
Hata
hivyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi anatoa wito kwa wananchi kutojihusisha na
shughuli haramu za ujangiri na biashara za nyara za serikali kwani ni uhalibifu wa rasilimali za taifa letu hasa
kwa manufaa ya vizazi vijavyo na pia amesisitiza
hatua kali za kisheria zitaendelea kuchukuliwa kwa wote wasiotii sheria pasipo
kushurutishwa.
Comments